Hatimaye Hawa Afanyiwa Upasuaji Salama Hali Yake Yaanza Kuimarika

Hatimaye Hawa Afanyiwa Upasuaji Salama Hali Yake Yaanza KuimarikaMsanii wa muziki Bongo Hawa amefanyiwa upasuaji baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa moyo.

Meneja wa WCB, Babu Tale ambaye yupo nchini India ameeleza kuwa atarejea wiki ijayo baada ya matibabu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Asante Mungu mgonjwa amemaliza salama hivi ameshazinduka na madaktari wametupa uhakika wa mgonjwa atakua salama na mpaka hivi sasa tumbo limeshaanza kupungua na Mungu akipenda baada ya wiki moja na nusu ataruhusiwa kurudi Dar," ameeleza.

"Hii ni hatua kubwa sana na mtihani unamkuta kila binadamu na mwenye kuutatua ni Mungu mwenyewe niwashukuru wote mlioweza kumuombea dua hawa mpaka hapa alipo na pia niendelee kuwaomba msiache kuomba dua," ameeleza Babu Tale.

Utakumbuka muimbaji Hawa alijizolea umaarufu mkubwa aliposhirikishwa na Diamond Platnumz kwenye wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nitarejea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad