Hawa Kufanyiwa Upasuaji Mkubwa wa Moyo Leo kwa Masaa Matano

Hawa Kufanyiwa Upasuaji Mkubwa wa Moyo Leo kwa Masaa Matano Msanii Hawa bado anaendelea kupatiwa matibabu nchini India ambapo leo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

Meneja kutokea WCB, Babu Tale ambaye ameongozana na muimbaji huyo hadi India ameeleza kuwa upasuaji huo utachukua saa tano. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Wapendwa tumuombee dua Hawa ameingia kwenye chumba cha upasuaji mkubwa wa moyo anasimamiwa na madaktari sita na wamesema watachukua saa tano kumaliza kila kitu," ameeleza Babu Tale.

Hawa alijizolea umaarufu mkubwa aliposhirikishwa na Diamond kwenye wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nitarejea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad