Ikiwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kikitarajia kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya hatma ya wabunge wawili, saed Kubenea wa Ubungo pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Anthony Komu, imetajwa wabunge hao walishaonywa kwa mara kadhaa.
Kwa mujibu wa mmoja wa kada maarufu wa Chama hicho ambaye amekuwa akitumika kukitetea chama kupitia mitandao ya kijamii, Yericko Nyerere ameandika tuhuma tano ambazo zimekuwa zikiwakibili wabunge hao wawili.
Kupitia mitandao yake ya kijamii kada huyo ameandika kuwa tuhuma ya kwanza inayowakabili wabunge hao ni, “miezi sita tangu apotee Ben Saanane huku chama na Watanzania nchi nzima wakiwa kwenye hekaheka ya kumtafuta Ben, na huku wakishinikiza serikali iharakishe kumtafuta Mtanzania mwenzetu, Saed Kubenea akishirikiana na Antony Komu aliyejitambulisha katika taarifa ya gazeti kama mjumbe wa Kamati kuu, waliandika kuwa Ben hajatekwa, yuko vijiweni kajificha tu, Mbowe anajua alipo”.
Tuhuma nyingine “baada ya Lissu kupigwa risasi na kukimbizwa Nairobi, huku Chama na umma ukiendelea na harambee ya kuchangia matibabu ya Lissu, Saed Kubenea na Antony Komu kwakushirikiana na watesi wetu, walianzisha kampeni ya kumchochea Lissu na kutengeneza mgogoro kati ya chama na Lissu, mpaka Lissu alipowashushua wakaingia mitini kabisa. Hili tu lilitosha Antony Komu ma Kubenea kufukuzwa katika Chama hiki.
“Antony Komu na Saed Kubenea wakijua wazi ni kosa kwa mujibu wa katiba ya chama, Wameanzisha ziara za kuzunguka mikoani kutengeneza mtandao wa kuasi chama huku wakisambaza habari za kuchafua uongozi uliopo madarakani kikatiba”.
“Huku wakijua ni mwiko kikanununi na kimaadili ya chama, Kubenea na Komu walipoitwa mbele ya mamlaka za kinidhamu za chama na kuonywa, katika hali ya kustaajabisha na kuonyesha wanatafuta kufukuzwa kwa nguvu, wakavujisha barua zao za kujieleza walizoandikiwa na chama kama hatua za kinidhamu”.
“Huku tayari wakiwa wameshaandikiwa barua za maonyo kama nilivyoeleza hapo juu, Kubenea na Komu hawakujali wala kusikia, Wakanaswa na teknolojia ya mzungu, Sauti (Audio) ya njama za kuwabambikia kesi viongozi wenzao na kupanga kuwapoteza baadhi ya wajumbe (Boniface Jacob), ikiwemo kumtengenezea kesi ya utakatishaji fedha Mwenyetiki wa Chama Mh Freeman Mbowe. (Rejea kusikiliza hiyo audi hapo chini).” alimaliza Kada huyo maarufu wa CHADEMA.
Leo saa tano asubuhi kamati kuu ya Chama hicho kinatarajia kutangaza uamuzi wa kuwachukulia hatua za kinidhamu wabunge hao ambao.