Hii ndio sababu ya Manula kuendelea kumkalisha benchi Dida


Kocha mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC Patrick Aussems ametoa sababu za kwa nini hamtumii mlinda mlango Deogratius Munishi “Dida” katika michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara. 

“Dida” ambaye alirejea nchini akitokea Afrika kusini mwezi Julai mwaka huu na kujiunga na mabingwa hao bado hajapata nafasi ya kucheza katika michezo ya ligi kuu, chini ya kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji. 

Aussems amesema hayo jana kwenye Uwanja wa Boko Veteran alipokuwa akikinoa kikosi chake kuwa “Dida” ana kiwango kizuri na ni miongoni mwa walinda milango wanne alionao kikosini, lakini kwa sasa anaona kuna haja ya kuendelea kumtumia Aishi Manula kutokana na kuwa na muendelezo mzuri anapokaa langoni. 

Amesema Simba bado ina kabiliwa na michuano mingine msimu huu, hivyo ana uhakika wa kumtumia “Dida” na walinda mlango wengine kikosini mwake kadri mazingira yatakavyomruhusu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad