Hiki Hapa Chanzo cha Moto Katika Jengo la Benjamin Mkapa Tower

Hiki Hapa Chanzo cha Moto Katika Jengo la Benjamin Mkapa Tower
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kuzima moto uliozuka kwenye gorofa ya tatu la jengo la Benjamin Mkapa tower, uliozuka majira ya asubuhi leo na kuzua taharuki kubwa kwa watumiaji wa jengo hilo.

Moto huo ulioanza kuwaka asubuhi ya leo Oktoba 4, 2018 katika ghorofa ya nne, umezua taharuki kwa watumiaji wa jengo hilo na viunga vyake.

Mkaguzi msaidizi wa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Elinimo Shang'a amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ilioanzia stoo, hivyo kutokana na uwazi katika chumba hicho moshi ulisambaa na kusababisha taharuki.

“Tumefika tumekuta wafanyakazi wamejitahidi kuudhibiti kwa kutumia vifaa vyao ili usisambae, tulichofanya ni kuuzima kabisa ili usilete madhara”, amesema Shang'a.

Amesema kuwa moto huo haujasababisha madhara kwa mtu yeyote lakini uchunguzi unaendelea kujua hasara iliyopatikana.

Tukio hilo lililodumu kwa muda wa dakika 45, ulizua taharuki na kusimamisha shughuli za watumiaji wa jengo la NSSF Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam pamoja na ofisi za jirani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad