Historia za Wachungaji 7 na Utajiri wao


Wengi huamua kuokoka na kufuata misingi ya kidini lakini wateule wachache huteuliwa kuwa wachungaji na kuchunga kondoo wa bwana watu hawa huwa na nguvu kubwa ya ushawishi.

Siku hizi kuwa mchungaji imethibitika kuwa ni kazi inayolipa kutokana na idadi kubwa ya watu watakaoamua kukuamini na kukufuata kama mchungaji wao.

Basi hapa nimekuandalia wachungaji watano maarufu na wenye mkwanja mkubwa zaidi hapa Afrika

Mchungaji Chris Okotie.

Huyu ni mchungaji mwenye vipawa mbalimbali ikiwa pamoja na mwandishi mzuri, mwanamuziki lakini pia ni mwanzilishi wa kanisa la ” Wakazi wa Mungu”, Chris Okotie ni moja ya wachungaji maarufu sana nchini Nigeria, amehitimu mafunzo ya sheria na kuamua kuanzisha kanisa lake, Chris amewahi kugombea nafasi ya urais bila mafanikio yeyote ni moja ya wachungaji tajiri sana wenye mapenzi mengi na magari ya kifahari yenye starehe, amewahi kumiliki gari aina ya Rangi Rover na Rols Royce Phantom, Pato lake linakadiriwa kuwa dola milioni 3 hadi 10 kwa pesa ya kitanzania ni bilioni za kutosha.

2. Mchungaji Mathew Ashimowolo

Huyu ni mchungaji kwenye kanisa moja huko Marekani, mwenye wafuasi wanaokaribia 12,000, Mchungaji huyu pia ni mtangazaji wa kipindi cha radio kinachofahamika kama ‘Winning ways” kinachorushwa katika stesheni  za radio mbalimbali zinazopatikna Afrika na Ulaya, Huyu jamaa yeye alibadili dini na kuwa mkristu akiwa na miaka 20 baada ya kifo cha baba yake. Jarida la Forbes limekadilia pato lake kuwa ni dola milioni 6 hadi 10 na kanisa lake linamiliki biashara inayoingiza pato la dola milioni 40. Mchungaji Mathew amewahi kufanyiwa uchunguzi juu ya mapato yake ya fedha na kukutwa anawatumia vibaya waumini wake na aliamriwa kurejesha dola 300,000 kama fidia kwa waumini wake.

3. Mchungaji T.B Joshua

Mchungaji huyu amepata umaarufu mkubwa Afrika nzima kufuatia Televisheni yake ya Emmanuel TV ambayo ni moja ya chaneli kubwa ya kikristo inayotazmwa zaidi barani Africa. Mbali na umaarufu huo Afrika bali ni mtu wa mitandao ya kijamii kwani anawafuasi milioni 2 kwenye ukurasa wake wa Facebook, Subscribers 800,000 kwenye You Tube kitu ambacho kinamfanya awe mchungaji maarufu sana anayefuatiliwa kupitia mtandao wa You Tube.

Pato lake si chini ya dola milioni 10 hadi 15, jarida la Forbes limewahi kumtunuku kuwa mchungaji wa tatu nchini Nigeria kwa utajiri mkubwa jambo ambalo baade lilipingwa na kanisa lake, hata hivyo taarifa za chinichini pia zilieleza Joshua amefanya manunuzi ya ndege binafsi iliyogharimu Dola milioni 60.

4. Mchungaji Uebert Angel

Mara kwa mara amekuwa akionekana akisafiri kwa helikopta, Mchungaji Uebert ni Rais na mwanzilishi wa Spirit Embassy, aliyejisajili kama mfanayabisahara mkubwa na anayeendesha biashara zake nyingi UK, Amekuwa akielezewa kuwa ni moja ya wachungaji wenye umri mdogo zaidi duniani, na kunukuliwa kuwa mwanamapinduzi ya mahubiri. Uebert amekuwa akiandikwa kwenye vichwa mbalimbali vya habari  Africa na Ulaya kwa miaka mingi kwa muujiza alioufanya 2014, Pato lake bado halijakadiliwa kufikia dola milioni kadhaa japokuwa ni mtu anayemiliki makazi mbalimbali na biashara kubwa zenye thamani ya dola milioni 25 pamoja na magari ya kifahari aina ya Range Rover, Lamborghini na  Rolls Royce yenye thamani ya dola milioni 5 kwa pamoja.

5. Enoch Adeboye



Mchungaji huyu alipewa heshima na nafasi kubwa katika kanisa la RCCG huko Nigeria mwaka 1981. Wakati huo alikuwa ni profesa wa somo la hesabu katika chuo kikuu cha Ilorin mpaka ilipofika mwaka 1984, mchungaji Enoch aliamua kuachana na uprofesa na kumtumikia bwana masaa yake yote .

Tangu Enoch Adeboye awe mfuasi wa kanisa la RCCG alifanya kazi kwa bidii kutanua kanisa hilo na baadae kupata umaarufu mkubwa duniani kote, Leo Enoch ana matawi zaidi ya 196 katika mataifa mbalimbali na ni moja ya wachungaji wenye ushawishi mkubwa sana hapa duniani na  mwenye utajili wa pato kubwa zaidi miongoni mwa wachungaji.

6. David Oyedepo

Mchungaji huyu ana pato sio chini ya dola milioni 150, ni mchungaji tajiri sana nchini Nigeria, Davidi alidai kuwa alitumiwa ujumbe na Mungu akiwa bado kijana mdogo akimtaka kusafisha dhambi za wanadamu kupitia imani yake ambayo ilimpelekea kufungua kanisa lake. Leo mchungaji Davidi ana wafuasi 50,000 katika kanisa lake lililonzishwa mwaka 1983 lenye makao makuu yake Logos.

Lakini unaambiwa mchunagji huyu pamoja na wafuasi wake wanamiliki nyumba kadhaa pamoja na ndege binafsi nne.

7. Shepherd Bushiri

Anfahamika kama ‘Major one’, muhubiri na mwanzilishi wa kanisa la ‘Enlightened Christian Gathering’ lenye wafuasi wengi hali inayomfanya sio tu kuwa muhubiri wa dini na siasa pia.

Sherphered Abushiri amewahi kufanya muujiza ambapo alimponya mtu mmoja aliyekuwa akisumbuliwa na Ukimwi pamoja na magonjwa mengine, japo muujiza huo ulifanya watu wengi wamkosoe jambo ambalo lilimfanya aamue kuua moja ya kanisa lake huko Botswana.

Pato lake linakadiriwa kuwa dola milioni 150, anamiliki magari ya kifahari pamoja na ndege binafsi yenye thamani ya dola milioni 37, anamiliki nyumba katika ameneo mbalimbali ya nchi za Afrika

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad