Huddah Monroe Amtaka Kenyata Kualalisha Bangi Kabla ya Kura ya Maoni

Huddah Monroe Amtaka Kenyata Kualalisha Bangi Kabla ya Kura ya Maoni
Huddah Monroe

MSANII maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe ‘amerusha kombora’ kwa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta akimtaka kuhalalisha matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi kabla hata ya kura ya maoni kuandaliwa.


Huddah ambaye wengi wanafahamu kuwa anatumia mmea wa bangi kama kiburudisho chake, aliibuka na kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni na kuandika; “Kabla ya kura ya maoni, tunataka bangi ihalalishwe. Ni nani aliye karibu na rais kwa sasa? Mfikishieno ujumbe huu.”

Mwaka jana, zaidi ya Wakenya 1,400 waliunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea wa bangi baada ya mtafiti Gwada Ogot kuwasilisha hoja ya ombi lake mbele ya Bunge la Seneti na kubainisha kwamba matumizi ya kiafya pamoja na utumizi wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa una faida nyingi.


Alisema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi lakini Sheria ya Kenya inapiga marufuku utumizi wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.

Mtafiti huyo ambaye amekiri kuvuta bangi wakati alipokuwa kijana amesema kuwa mataifa mengi katika bara Ulaya na Asia pamoja na majimbo kadhaa nchini Marekani yamehalalisha utumizi wa Marijuana. Aliorodhesha Colombia, Mexico, Jamhuri ya Czech, Costa Rica,Ireland ,australia, Jamaica na Ujerumani kama mataifa yaliohalalisha matumizi wa mmea huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad