Huyu ndio Mwanadada Hurrem Sultana wa Tamthilia ya Sultan

WASIFU WAKE.
Huyu ndio Maryem Sarah Uzerli almaarufu Hurrem Sultan wa tamthilia ya Sultan (muhteşem yüzyıl) inayoonyweshwa katika king'amuzi cha azam tv kupitia chaneli ya Azam Two.

Meryem ni muigizaji na mwanamitindo mwenye asili ya nchi mbili ambazo ni Ujerumani na Uturuki. Alizaliwa tarehe 12/08/1983 katika mji wa Kassel-Ujerumani.

Baba yake ni mturuki na Mama yake ni Mjerumani.Amekulia zaidi katika mji aliozaliwa wa Kassel, ila kwa sasa makazi yake ni katika jiji la Berlin-Ujerumani na Istanbul-Uturuki.

Lugha anayomudu kuizungumza kwa ufasaha ni Kijerumani, lakini pia anamudu kuzungumza Kituruki na Kingereza.
ndugu zake wa damu aliozaliwa nao kwa baba na mama ni watatu, makaka wawili na dada mmoja.

Ujuzi wake katika uigizaji aliupata katika shule kongwe ya masuala ya Sanaa za maigizo ya Schauspiel Studio Frese iliyopo katika mji wa Humburg. Alijiunga na masomo yake ya sanaa mwaka 2000 na kuhitimu mwaka 2003.

Baada ya kuhitimu masomo yake, aliamua kushiriki sanaa za majukwaani nchini ujerumani akiwa kama muigizaji mchanga.

Sambamba na kushiriki katika Tamthilia mbalimbali, Tamthilia pekee iliyompatia umaarufu mkubwa ni Sultan (muhteşem yüzyıl). Mtu pekee aliyempa shavu la umaarufu huu si mwingine bali ni mwanamama mtunzi wa tamthilia hiyo Meral Okay pale alipomchagua acheze kama muigizaji kinara kupitia character ya Hurrem Sultan.

Mara tu alipopata nafasi hiyo, aliondoka Ujerumani na kuhamia Uturuki. akiwa katika jiji la Istanbul-Uturuki ilimzalimu kuishi hotelini miaka miwili ili akamilishe zoezi la uchukuaji picha wa Tamthilia hii ya Sultan.

Ifahamike tu kwamba, iliwachukua miezi nane waandaji wa tamthilia ya Sultan kumtafuta mtu sahihi ambaye angemudu vizuri kucheza character ya Hurrem Sultan. na bahati hiyo ikamdondokea Bibie Meryem Uzerli.

Uwezo wake wa uigizaji aliounyesha katika Tamthilia hii, umemfanya ajishindie tuzo kemkem ikiwemo Golden Butterfly Award aliyoshinda mwaka 2011 na Golden Butterfly Award aliyoshinda mwaka 2012 kama muigizaji bora.

Moja kati ya kituko alichowahi kukutana nacho katika maisha yake ya ustaa ni pale mwaka 2014 alipoalikwa na familia moja ya kitajiri huko Mashariki ya Kati.

Familia hii ilimtumia mualiko wa kushiriki naye chakula maalum. Ilihaidi kumpatia euro 500,000, takribani fedha za Kitanzania 1,326,394,699 (billioni moja na milioni mia tatu ishirini na sita, laki tatu na tisini na nne elfu, mia sita tisini na tisa), endapo tu kama angekubari ombi lao.

Kwa kujiamini, Maryem aliwajibu kuwa yeye huwa hana kawaida ya kukubari mialiko ya namna hii na ili akubari mualiko huo, Familia hiyo igawe fedha hizo kwa Taasisi tatu za Kituruki zinazojihusisha na kulea Watoto wenye mahitaji maalumu.

Kwa jeuri ya fedha, Familia ile ilimtuma mtu wao imwambie Maryem kuwa wataongeza dau maradufu. na kweli dau liliongezwa.

Mwisho wa siku Maryem alikubari mualiko na alienda Mashariki ya Kati kushiriki kula chakula maalumu pamoja na familia ile ya Kitajiri.

Makala hii imeandikwa na mimi Jamvini Storyteller kwa kupitia vyanzo mbalimbali vya mitandao ya Habari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad