Idadi ya Waliofariki Duniana Tetemeko la Ardhi Indonesia Yafika Watu 832

Idadi ya Waliofariki Duniana Tetemeko la Ardhi Indonesia  Yafika Watu 832
Takriban watu 832 wameuawa baada ya tetemeko kubwa la ardhi na tsunami kupiga kisiwa cha Indonesia cha Sulawezi, kwa mujibu wa shirika la majanga la kitaifa.

Juhudi za kuwatafuta manusura zinaendelea na idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda pakubwa maeneo mengi ambayo kufikia sasa hayajafikiwa na waokoaji yakifikiwa.

Shirika hilo liloongeza kuwa eneo lililoathiriwa lilikuwa kubwa kuliko iliyodhaniwa.

Watu wengine waliripotiwa kukwama kwenye vifusi vya mango yaliyoporomka siku ya Ijumaa.

Indonesia yakumbwa tena na tsunami
Tetemeko hilo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi ya hadi urefu wa miata 6.

Waokoaji wamekuwa wakichimba kwa mikono wakiwatafuta manusura kwenye mji wa Palu.

Vikosi vya uokoaji vinajaribu kuwafikia mamia ya watu ambao inawezekana wakawa hai katika mji wa Palu ambao miundombinu yake imeharibika vibaya huku wengi wao wakitajwa kukwama katika maduka na majumba makubwa.

Sehemu kubwa ya mji wa Palu imeharibiwa vibaya huku dalili za kuwapata walionasa wakiwa hai zikianza kufifia.

Daraja hili liliharibiwa na tsunami iliyosababishwa na tetemeko hilo
Katika ziara yake kwenye mji wa Palu Rais wa Indonesia Joko Widodo, amewaambia viongozi wa eneo hilo kuwa serikali kuu itatoa mahitaji yote muhimu ili matengenezo mapya ya mji huo yaweze kufanyika.

''Hakika hii ni hali ya dharura kama ilivyo ya Lombok. Kutakua na ugumu wakati, kwa siku moja au mbili na ni kazi kubwa. Uelekeo wa Barabara hii haipo imefungwa, ata uwanja wa Ndege haufanyi kazi ipasavyo," amesema.

"Vituo vya kuzalisha umeme pia vimeharibiwa, na kati ya saba ni viwili tu ndivyo bado vinafanya kazi na wasambazaji wa mafuta wasingeweza kuyafikia maeneo kutokana na kuharibika kwa barabara. Lakini tayari tumeagiza kila kitu kama mafuta, na wasambazaji watafika siku mbili kuanzia sasa.

"Na vifaa vyote vizito vitakuja usiku wa leo, ili tuweze kuvitumia kesho pamoja na ahueni ya misaada kama vile chakula na maji safi.Baada ya kuona kila kitu kinafanya kazi kama kawaida tutaingia kwenye hatua kujenga na kuzirekebisha nyumba hizo. Na Serikali itawaaidia kama tukivyofanya Lombok."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad