Ifike Mahali Tuache Kuwafananisha Diamond na Ali Kiba, Tunakosea Sana

Waswahili wanasema huwezi kuijua chungu kama hujawaonja tamu. Ni kawaida yetu binadamu kupenda kulinganisha vitu. Tusipojilinganisha watu, tutawalinganisha wengine. Tusipolinganisha vitu, tutalinganisha wanyama.

Mwisho wa makala haya msomaji utatakiwa kutoa maoni yako. Je, ni sahihi kuendelea kuwalinganisha wanamuziki Diamond Platnumz na Alikiba.

Hata hivyo, kuna wakati inabidi tukubali tu kuwa wengine wapo katika anga ya peke yao, kama ni michezo basi tunasema wanacheza katika ligi za peke yao.

Kwa zaidi ya miaka mitano sasa mashabiki wamekuwa wakiwalinganisha wanamuziki Diamond Platnumz na Alikiba. Je, ni sahihi kuendelea kuwalinganisha wanamuziki hawa hata sasa?

Kwanza tukubali kuwa wote wana kipaji cha uimbaji, lakini kipaji pekee hakitoshi kuwalinganisha na ndio maana wasanii kama Benpol, Belle9 hawajaunganishwa katika vita hii.

Kwa mfano Diamond ameshafanya kazi na wasanii zaidi ya watano wakubwa duniani.

Wasanii hao ni Rick Ross, Omarion, Morgan Heritage, Mr Flavour, Mohombi na wengine wengi barani Afrika na Alikiba ameshirikiana na M.I kutoka Nigeria na R Kelly akiwa na wasanii wengine saba katika programu ya One8.

Kingine ni kwamba Diamond, hutoa wimbo mpya karibu kila mwezi na Alikiba kwa wastani huachia wimbo mmoja kwa mwaka.

Diamond analalamikiwa kwa kutoa nyimbo nyingi na Alikiba kwa kutoa chache. Lakini kipi bora kwa msanii ni kutoa nyimbo au kukaa kimya? Msomaji kuwa mwamuzi katika hili.

Harmonize ambaye anatajwa kuwa msanii anayemfuatia Diamond kwa utajiri yupo chini ya WCB.

Lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond inasimamia wasanii wakubwa nchini wakina Ray Vanny, Lavalava, Queen Darlin na Mbosso wakati Kings Music ya Alikiba ndio kwanza ina wiki moja tangu ianze kufanya kazi ikiwa na wasanii wanne.

Pamoja na mafanikio katika muziki, Diamond amekuwa akilalamikiwa kwa kuwadhalilisha wanawake hasa kuwatumia kama vibwagizo katika nyimbo zake, hata Alikiba anaingia katika mkondo huu ingawa huwa haweki mambo yake hadharani hasa ikitolewa mfano kuwa amekuwa na watoto kutoka kwa wanawake tofauti.

Je, kuna haja ya kuendelea kuwalinganisha wasanii hawa?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad