IGP Sirro Aapa Kuwanasa Waliomteka Mo Dewji Wakiwa Hai au Wamekufa

IGP Sirro Aapa Kuwanasa Waliomteka Mo Dewji Wakiwa Hai au Wamekufa
Polisi nchini Tanzania wamesema watafanya kila wawezalo kuwatia nguvuni watu waliomteka na kumshikilia bilionea Mohammed Deji, Mo, kwa siku tisa.

Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amewaambia waandishi wa habari hii leo Oktoba 20 kuwa kuachiwa kwa Mo ni mwanzo wa kuwanasa wahalifu hao na kjuahidi kuwapata wakiwa wazima au wamekufa.

"Mbio ukizianza sharti uzimalize. Huu ni mwanzo tu. Hao wahalifu wanaotaka kuchafua jina la nchi yetu lazima tuwatie nguvuni."

Mo Dewji: Polisi Tanzania wanasema watekaji walitaka pesa
Polisi watambua gari lililotumika utekaji wa Mo Dewji
Gari alilotekewa Mo Dewji limesajiliwa Msumbiji
Sirro amesema upelelezi umeimarishwa kwa kushirikiana na mtandao wa polisi wa kimataifa Interpol.

"Nataka niwaambie (wahalifu) yawezekana wananisikiliza hivi sasa kuwa, popote watakapoenda tutawanasa. Wakienda Afrika Kusini tunao, Kenya tunao, Uganda tunao hata Msumbiji, popote pale tutawakamata maana tayari tunaushirikiano na wenzetu."

IGP Sirro amesema taarifa za kiupelelezi alizozitoa jana juu ya gari lilotumika kumteka Mo Dewji Alhamisi ya wiki iliyopita na dereva aliyekuwa analiendesha lilipoingia Tanzania limesukuma watekaji hao kuogopa na kumwachia huru Mo.

"Tayari tunamjua dereva, tunamjua mmiliki wa gari...tumeweka wazi picha za gari. Wkaona hawana namna zaidi ya kumwachia tu. Lakini kama nilivyosema nitawapata na kuwagonga na sheria wakiwa wazima au wametangulia mbele ya haki (wamekufa)."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad