IGP Sirro: Watekaji wametelekeza Gari na Silaha 4 Ikiwemo Moja ya Kivita

IGP Sirro: Watekaji wametelekeza Gari na Silaha 4 Ikiwemo Moja ya Kivita
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amezungumzia tukio la kupatikana kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Dewji kutoka kwenye mikono ya watekaji na kusema imebainika nia ya watekaji hao walitaka awapatie pesa.



Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2018, Sirro amesema; “Nimeambiwa kwamba waliomteka Mohammed Dewji amesema walimwambia walitaka pesa, alipowauliza shilingi ngapi hawakusema, aliwapa simu waongee na baba yake lakini waliogopa kwa sababu wanafahamu ulinzi wetu ni imara tungewakamata.



“Mohammed Dewji amesema watekaji hao walikuwa na wasiwasi sana, baada ya kuona hawawezi kutoka, njia pekee ni kuliacha hili gari hapa majira ya saa saba usiku, MO aliwapa taarifa wazazi wake wakaja kumchukua.



“Watu wetu wako kwenye hizo nchi, tunataka kuwaonyesha ukizoea Tanzania siyo mahali salama, kama walizoea kwenye nchi zao siyo hapa kwetu. Kuacha gari hii na silaha siyo mwisho wa upelelezi. Najua kuna Mtanzania mmoja, tuwapate tuzungumze nao lugha nzuri ‘bro’,



“Watekaji hao walitaka kuichoma hii gari kupoteza ushahidi, wakajikuta mwisho wa siku wana mashaka na hilo. Inasemekana walikuwa wakizungumza Kiingereza na Kiswahili cha hovyo hovyo, siwezi kusema wametoka nchi gani mpaka pale tutakapowatia mbaroni,” alisema Sirro.



Mo Dewji alitekwa alitekwa alhamisi iliyopita, Oktoba 11, 2018 katika gym ya Hotel ya Colosseum iliyopo Oysterbay jijini Dar es salaam na kupatikana usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Gymkana baada ya kutelekezwa na watekaji hao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad