Injinia Aliyeokolewa Siku ya 3 Akiwa Hai Katika Ajali ya MV Nyerere Asimulia Alivyonusurika

Injinia Aliyeokolewa Siku ya 3 Akiwa Hai Katika Ajali ya MV Nyerere Asimulia Alivyonusurika
Jina la Injinia Augustine Cherehani lilianza kuvuma katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania siku tatu baada ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake katika ziwa Victoria kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara.

Injinia Augustine Cherehani katika kile kilichowaacha wengi vinywa wazi aliokolewa wakati tumaini la kupata walio hai likiwa limesha malizika.

Injinia ambaye ndiye fundi mkuu wa kivuko hicho kilichopinduka Mwezi wa tisa tarehe 20 mwaka wa 2018 na kuua watu zaidi ya 225, alimsimulia mwandishi wa BBC Eagan Salla mkasa mzima.

'Siku kama siku nyingine'
Siku ya tukio Injinia anasema ilkuwa siku kama siku nyingine lakini kwao kwa misingi ya usafirishaji ilikuwa siku ya kazi kubwa kwani ilikuwa ni siku ya gulio eneo la Bugorora.

Kawaida wakazi wa kisiwa cha Ukara hufurika gulioni kujipatia mahitaji mbalimbali na siku hiyo ilikuwa vivyo hivyo.

Kabla ya safari kama kawaida alikagua chombo (MV Nyerere) zikiwemo Injini zake mbili mpya na kujiridhisha kuwa chombo kilikuwa tayari kwa safari kutoka Bugorora (Ukerewe) kueleka Bwisya (Ukara)

Baada ya kuwasha Injini alimruhusu Nahodha kuianza safari ambayo kwa kawaida huchukua wastani wa dakika arobaini na tano (45) hadi saa moja.

Kawaida na kwa mujibu wa mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini nchini Tanzania, Sumatra, Mtaalamu huyu ana wajibu wa kutoa mwongozo kwa nahodha kwamba chombo kiende kasi gani kutokana na hali ya Injini na mzigo kilio beba jambo ambalo injinia Cherehani siku hii alilifanya mwenyewe kutokana na msaidizi wake kutokuwa kazini.

Baada kukamilisha wajibu huu wa muhimu, Injinia huyo mwenye miaka 53 mkaazi wa Magu Masanza jijini Mwanza alirejea katika chumba cha injini na kuketi katika kiti chake kuhakikisha hali ya injini zake ni shwari mpaka Mv Nyerere itakapo kita nanga.


Augustine Cherehani: Injinia aliyenusurika baada ya kuzama MV Nyerere
''Ninacho kumbuka ni kwamba nilijikuta niko chini ni kama mtu kapigwa ngwara''

''Ninacho kumbuka ni kwamba nilijikuta niko chini ni kama mtu kapigwa ngwara''
Augustine Cherehani, Injinia mkuu MV Nyerere
Mara hii MV Nyerere ilisimama bila ya kukita nanga lakini pia injini zake ambazo amekuwa akizikagua mara zote, safari hii zilikuwa juu na yeye chini jambo ambalo si la kawaida, ndipo alipogundua hali si shwari hata kujisema moyoni ''hii ya leo nayo ni kali''.

Maji yaki panda kasi ya wastani tayari yalisha mvuka kiunoni lakini Injini tiifu za Mv Nyerere bado zilikuwa zikifanya kazi kabla ya kumwaga oili na kuzima.

''Injini zile zimezimika, wakati ule zimeshapata moto, na sasa zikaanza kupoozwa na maji kwa kweli ile dakika ya kwanza mpaka ya ishirini ilikuwa ni kazi kubwa sana na nilihisi naweza kufa mapema sana kwa moshi kabla ya maji''.

Kiza kinene na utulivu wa mauti, Injinia huyu baba wa watoto wanne wasichana wawili na wavulana wawili aliomba kimoyo moyo na kumwambia Mungu, anajua 'yeye ni mwenye dhambi ikiwa Mungu hata ona huruma kwake basi aone huruma kwa watoto wake alio walipia kwenda kwenye makambi ya Kisabato kuutafu tafuta uso wa Mungu anaye mtumainia'.

Injinia ni Cherehani ni baba wa watoto wanne wasichana wawili na wavulana wawili, ambayo walikuwa moyoni mwake wakati wote wa mkasa huo
Jua linachomoza kwa walio nje ya MV Nyerere, lakini simanzi kwa wakazi wa wilaya ya Ukerewe, Tanzania inashusha bendera yake nusu mlingoti, hili si jambo la kawaida hakika taifa hili kubwa Afrika ya mashariki liko katika maombolezo.

Raisi John Pombe Magufuli anatuma salamu za pole na maombolezo salamu ambazo injinia Cherehani hazipati ila kwa uzoefu na utaalamu wa kibaharia anajua taifa linalia.

Kwake kiza kinaendelea na mara hii maji yanelekea kifuani, usiku wa pili usiku ambao ulikuwa na ndoto nyingi za mauti, anaposikia sauti za waokozi nje yeye anaendela kugonga akiwa na tumaini atasikika.

Mtalamu huyu anagonga kitaalamu , 1 2 3 ishara za kibaharaia na mabaharia wenzake wamsikia na kumgongea 1 2 3 anashusha pumzi na kuamini huenda aka uona tena uso wa Mke wake na watoto wake wapenzi.

Lakini si leo maana punde kimya kinatawala na yeye anajua sasa ni usiku umeingia, siku ya tatu bila maji wala chakula.

Anaposikia sauti za waokozi anaendela kugonga, 1 2 3 kama alivyofundishwa katika mafunzo ya ubaharia na Mungu si Athuman maana safari hii anauona mwanga wa kurunzi ya mzamiaji na yeye ana mrahisishia kwa kufuta weli chafu iliyotapakaa juu ya maji.

''…namshukuru Mungu alinipa uvumilivu nikasema kwamba kama ni kifo na kinikute hapa hapa".

Haki miliki ya pichaSTEVE MSENGI, AFISA HABARI WILAYA YA UKEREWE
Hakika subira huvuta kheri, mzamiaji huyu alikuja mara tatu na safari hii alimgonga begani na kumwambia ''bwana nimekuja kukuchukua lakini kabla ya hapo naomba nikupe darasa, kama utafanya mchezo nitakutoa marehemu"

Baada ya dakika kadhaa za hofu na kukata tamaa ndipo kamera za waandishi wa habari zilipo mmulika, na waandishi hao kuandika: 'Injinia Mkuu wa MV Nyerere aokolewa siku tatu baada kuzama kwake akiwa amejipaka weli chafu'.

Kati ya Mwaka 2009 hadi 2017 Mwezi wa tano Injinia huyu anayeliona jua baada ya siku tau alihudumu kama injinia mkuu katika vivuko vya serikali ya Tanzania kigongo ferry kabla ya kuhamishiwa Ukerewa kukihudumia kivuko cha MV Nyerere mwezi wa tano mwaka 2017 hadi siku ya mkasa huu usio sahaulika.

''Kuna namba yoyote unayo ikumbuka nikamwambia ni ya mke wangu, unaweza kunitajia nimwambie? ndipo nilipo mtajia, akanipa kuongea naye aliposikia sauti yangu akaniambia inabidi umwombe Mungu sana sisi tayari tulishaweka msiba hapa''.

Kwa Picha: Sehemu za ndani za gari lililotumika kumteka Mo Dewji

Wanasiasa wanacheza karata mjadala wa mageuzi ya katiba Kenya

Baada ya kuokolewa, Injinia huyu alipatiwa huduma ya kwanza katika kituo cha afya cha Bwisya na kuchukuliwa kwa helikopta ya polisi kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando na kupatiwa matibabu kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.

'Ila mpaka sasa bado na hudhuria kliniki katika hospitali hiyo'.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad