Irene Uwoya Achoshwa na Maumivu ya Mapenzi "Maisha Magumu Bado Mapenzi Yakusumbue achana Naye"

Irene Uwoya Achoshwa na Maumivu ya Mapenzi "Maisha Magumu Bado Mapenzi Yakusumbue achana Naye"
Muigizaji Irene Uwoya ametoa ushauri kuhusiana na suala zima la mapenzi na kudai kuwa suala hilo limemfika kooni na hivyo kuamua kufunguka na kutoa ushauri juu ya watu wanaofanywa watumwa kwenye dunia ya mapenzi.

Kupitia ukuarasa wa instagram wa Irene Uwoya ameandika ujumbe wa kuwataka wale wote ambao wanafanywa watumwa kutokana na kumpenda mtu halafu kwa upande mwingine mtu huyo anakuchukilia poa amewataka wafunike sura na waendelee na maisha mengine.

“Mapenzi au kumpenda mtu kusikufanye uwe mtumwa ukiona unampenda mtu halafu anakuchukulia powa achana nae. Maisha yasahiv sio yakujipendekeza au kulazimishana mtu uwaze Maisha Magumu bado mapenzi yakusumbue?achaaa ujinga na usikubali kuwa mtumwa…wewe funika sura fanya kama uwoni#achaunafkiuwendembinguni“


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad