Jack Wolper "Wanaume Wametufanya Sisi Mastaa wa Kike Kama Madaraja"
0
October 11, 2018
MREMBO kutoka Bongo Movies, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa wasanii wengi wa kike mawazo ya kuolewa yameshafutika mioyoni mwao kwa sababu wanaume wengi wamekuwa wakiwatumia kama madaraja.
Akizungumza na Amani, Wolper alisema kuwa mara nyingi wanaume wamewachukulia wasanii kama daraja la kusonga mbele au kukuza majina yao lakini siyo mapenzi ya dhati. “Ni hivi mastaa wengi hasa kwenye tasnia ya uigizaji wameamua kufanya maisha yao wenyewe na kusahau kabisa kama kuna jambo la kuolewa na ndiyo maana unaweza kukaa hata miaka mitano bila kusikia msanii wa kike ameolewa,” alisema Wolper.
Miaka ya hivi karibuni, wasanii wengi wa kike wamekuwa wakizalishwa na kulea watoto waozalishwa peke yao, baada ya kuachwa solemba na wanaume zao.
Tags