Watu wengine 14 wamejeruhiwa huku 7 wakiokolewa baada ya jengo hilo lililokuwa linajengwa kuanguka huko Barani, Malindi asubuhi ya leo Oktoba 26
Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya Watu wengine kadhaa wamekwama ndani ya kifusi cha Jengo hilo huku taratibu za uokoaji zikiendela
Inaelezwa kuwa Jengo hilo lilikuwa kwenye mkakati wa kubomolewa baada ya kubainika kuwa lilijengwa bila kufuata sheria
Mwezi Juni mwaka huu, Watu watatu walifariki dunia baada ya jengo la ghorofa 5 kuanguka jijini Nairobi huku wengi wawili wakifariki jijini humo baada ya jengo lingine la ghorofa 7 kuanguka