Jerry Muro aomba msaada

Jerry Muro aomba msaada
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amependekeza kujengwa kwa choo kipya katika shule ya msingi Selian ambayo hivi karibuni ilisababisha watoto 65 kunusurika kifo baada ya choo cha shule hiyo kubomoka.

Kupitia taarifa iliyotumwa na Mkuu huyo wa Wilaya Jerry Muro amesema zoezi la uokoaji limeshakamilika na sasa wanaomba msaada wa milioni 25 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa choo kipya kwa ajili ya wanafunzi hao.

“Tunaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya choo kwa watoto wetu, tumeazimia kujenga choo aina ya Swashi, ambacho hakitakuwa na shimo katika eneo la maliwato na badala yake shimo litajengwa pembeni Kabisa ya choo.” Amesema Jerry Muro.

Aidha Jerry Muro amesema “gharama zinaonyesha ni shilingi milioni 25 ambazo zitajenga choo cha matundu 20, tunaomba michango ya vifaa, michango ya fedha na michango ya nguvu kazi tusaidiane hata kama haupo Arumeru''.

Jerry Muro ameelekeza kufuatwa kwa vigezo maalum vya ujenzi wa choo kama inavyotakiwa na ramani za halmashauri ili kuepuka maafa ya mara kwa mara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad