Jeshi la Polisi wafunguka kifo cha Mama mjamzito

Jeshi la Polisi wafunguka kifo cha Mama mjamzito
JESHI la polisi mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya jana wamekanusha madai kuhusika na kifo cha mama mja mzito kilichotokea majira ya saa1.20 Septemba 29 katika kijiji cha Komarera ambacho hapo awali ilidaiwa kuwa chanzo chake kilisababishwa na kugongwa na gari la polisi lenye namba za usajili PT 1010 Toyota L/Cruicer ambalo lilikuwa  likiendeshwa na Dereva wake G,7113 PC Simion Mauki.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu kamanda mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya SSP Hassani Maya ambaye pia ni mpelelezi wa makosa ya jinai katika  mkoa huo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kilitokana na mwendesha pikipiki kushindwa kumdu usukani na kusababisha ajali na kuua mama mja mzito na kujeruhi mwingine mmoja kwa hali hiyo gari la polisi halikuua.

"Septemba 28,2018 majira ya saa 1.20 katika barabara itokayo kijiji cha Nyamwaga kwenda kijiji cha Nyansangero katika kitongoji cha Komarera kijiji cha Gokemange kata ya Nyamwaga gari la polisi lenye namba za usajili PT 1010 Toyota LCruser likiendehswa na askari namba G,7113 PC Simion Mauke liligongana na pikipiki yenye namba za usajili MC 992 BEW aina ya Sanlg likiendeshwa na dereva aitwaye Peter Joseph mkazi wa kijiji cha Kimusi na kusababisha kifo kwa abiria wa pikipiki aitwaye Mariamu Petero mkazi wa Kimusi na kusababisha majeraha kwa abiria wa pili aliyekuwa abiria wa pikipikihiyo aitwaye Otaigwa Mwita"alisema Maya.

Maya aliongea kuwa  majeruhi huyo amejeruhiwa mguu wake wa kulia na amelezwa katika hospitali ya Wilaya Tarime ambayo inamilikiwa na halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara na hali yake ni mabaya.

Maya ameongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ini mwendokasi wa mwendesha pikipiki uliomfanya kushindwa kuimdu pikipiki na kujibamiza pembeni mwa gari la polisi.

Kwa upande wake mrakibu wa jeshi la polisi Tarime na Rorya,Ally Shaali alisema kuwa mwendesha pikipiki huyo hakuwa na mafunzo ya udereva na wala hakuwa na leseni kwa hali hiyo alikuwa anatumia uzoefu katika kuendesha ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka  waendesha vyombo vya moto kuzingatia elimu ya mafunzo ya usalama barabarani pamoja na kuwa na leseni

Jeshi la polisi linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili wa  shule ya sekondari Itiryo kwa kosa la kupatikana na pombe haramu aina ya Gongo ndani ya nyumba anayo lala kwa matumizi ya kuuza na kujipatia kipato.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu kamanda mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya,SSP Hassani Maya ambaye pia ni RCO,mpelelezi wa makosa ya jianai Tarime na Rorya alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni,Mwita Makubo (15) mkazi wa kijiji cha Itiryo kata ya Itiryo.

Maya aliongeza kuwa mwanafunzi huyo alikutwa na askari waliokuwa wakifanya msako wa kutafuta madawa ya kulevya pamoja na pombe haramu hapo Septemba 29,2018  ambapo walifanikiwa kukuta ndani chumba chake cha kulala  pombe ya moshi lita Nnee zikiwa zimehifadhiwa tayari kwa kuuzwa.

Pia Maya amesema kuwa katika msako huo polisi walifanikiwa kukamata lita 129 za pombe ya moshi katika maeneo mbalimbali na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

“Jeshi la polisi wakiwa katika msako wamefanikiwa  kukamata lita 129 za pombe haramu ya moshi katika maeneo mbalimbali na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika”alisema Maya.

Tarehe 29,09,2018 majira ya saa10.33 katika kitongoji cha Nyamunsi kijiji cha Korotambe asikari polisi wakiwa katika msako walifanikiwa kuwakamata Magebo Chacha,Amos Magaigwa na Nchagwa Chacha wakiwa na pombe ya moshi lita 10 wote wakazi wa kijiji cha Korotambe na wote ni wanywaji na wauzaji aliongeza kusema.

Wengie waliokamatwa katika tukio hilo ni pamoja na Kimune Meremo wa kijiji cha Kiongera ambaye alikamatwa akiwa na pombe ya moshi ndani ya nyumba yake lita 115 aliyokuwa ameiifadhi katika madumu ya ita 20 ya kupikia tayari kwa kuuzwa na kutumiwa.

Jeshi la polisi Tarime na Rorya linatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na biashara haramu ambazo zimepigwa marufuku na serikali badala yake wafanyew biashara halali ya kuwaingizia kipato.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad