Jeshi la Uganda limezindua mifuko ya kondomu katika kambi yake ya kijeshi ya UPDF Bombo iliyopewa kibwagizo cha usiende nyama kwa nyama.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Brigedia Leopoldo Kyanda amesema mwanajeshi hawezi kutekeleza wajibu wake ipasavyo bila wenyewe kujilinda kutokana na maambukizi ya zinaa na hususan virusi vya ukimwi.
Kondomu hizo zimepewa jina Ulinzi na zinatarajiwa kusaidia katika juhudi za kupunguza kuenea kwa virusi vinavyosababisha Ukimwi.
Kitengo cha kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi jeshini kilizindua nembo hiyo mpya kwa ushirikiano na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali.
Jeshi la Uganda Lazindua Kondomu Zenye Kibwagizo ‘Usiende Nyama kwa Nyama’
0
October 04, 2018
Tags