John Heche Alaani Kitendo cha Wanachama wa CHADEMA Kukamatwa Wakiwa Lodge


Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amelalamikia hatua ya jeshi polisi wilayani bariadi kuzuia mkutano wa ndani wa chama hicho ambao ulilenga kutoa mafunzo kwa wanachama wake kuelekea uchaguzi.

Kwa mujibu John Heche amesema chama hicho kinaendesha mafunzo kwa wanachama wake ambao wataenda kusimamia suala la uchaguzi kwenye ngazi ya msingi hivyo wamehuzunishwa na jeshi la polisi kuzuia mkutano wao licha ya kuwa wameshatumia gharama kuandaa.

"Sisi tuna uchaguzi ndani ya chama chetu kwa hiyo tunatoa mafunzo kwa viongozi wetu wa kanda mbili za Viktoria na kanda Serengeti ni jinsi gani wanaenda kutoa mafunzo ya kusimamia uchaguzi wilayani, lakini ghafla  watu wetu wa mafunzo wamefika wamezuiliwa." Amesema John Heche

"Mkuu wa wilaya kaitisha mkutano, kasema haitaki kuiona CHADEMA wilayani kwake, lakini jana akaenda kukamata baadhi ya wanachama wetu waliokuwa wamelala lodge pamoja na wamiliki kwa sababu gani wameruhusu wanachama wetu kulala kwenye lodge, lakini kiujumla ni vikao vya ndani ambavyo Rais ameruhusu." Ameongeza John Heche.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad