Julius Nyerere: Tunao Wanasiasa Wana Tabia za Kimalaya Malaya, Heshima yao inauzwa na ina bei (Mercenary)



Nlikuwa nasikiliza hotuba ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa Julai 22 mwaka 1967 Baada ya kuwapokea Vijana waliotembea kwa Miguu kutoka Moshi.

Alikuwa anaongelea kuhusu wanasiasa kununulika, Yaani hawa wananunulia na kusaliti vyama vyao au jamii iliyowachagua kwa vipande vya pesa akawaita ni Mwanasiasa Malaya ambao wao wanajali hela tu kama mercenary.

Nikaona inaendana na Wakati huu tulionao wa wanasiasa kuhama vyama ambapo inadaiwa baadhi yao wananunuliwa na wengine wanahama kwa utashi wao.

Hapa chini namnukuu alichokionge kuhusu wanasiasa wanaoambatana na mtu kisa tu wamepewa hela.

Anaanza kwa kusema, "Unakuta mtu anafuatana nalo hadi unajiuliza, huyu anafuatana nalo kwanini? Manake si heshima huyu kuandamana na yule, lakini unagundua anaandamahela. Hii ni tabia ya Kimalaya malaya. Na tunao wanasiasa wenye tabia ya Kimalaya malaya namna hii, wananunulika, heshima yao inauzwa, ina bei. Anakuuliza anaona... unasema fanya kitendo kadhaa ambacho ni kitendo cha aibu, lakini anakuuliza ngapi bwana?, Ukitoa bei ukimlipa basi, anakubali. Mwanasiasa ana tabia ya kimalaya malaya.

Mtu mwenye tabia ya kimalaya malaya ananunulika anafikiri kila mtu ananunulika. Kwahiyo anatoka anaenda kwa watu wengine, anadhani watu wengine wanaweza kufanya mambo ya aibu aibu ambayo hayana heshima..halafu anajuta, anajuta.

Kuna majeshi duniani humu yanaitwa Majeshi ya mercenary, yalikuwa hapo Congo, wengine ni vijana wadogo mnajua mercenary. mercenary ni mtu anafanya kazi kwa malipo, kwa pesa tu. Sababu yake kufanya kitendo kile ni pesa tu. Ukimuuliza kwanini unafanya hivi? anakujibu nalipwa.

Na hajali nani anayemlipa. INawezekana nchi mbili adui zinapigana hii na hii, anaweza kwenda kwa hii akasema mtanialipa? Kama hamuwezi kumlipa atawapigania hawa wengine kuua hawa. Yeye hana upande, anajua pesa tu. Maaskari hawa wanaitwa mercenary... anajua pesa tu, ni Malaya Malaya tu. Yupo tayari kuua au kuchukua hatari ya kuuawa sababu ya pesa tu. Askari wa kawaida yupo tayari kuua au kufa kwa sababu ya heshima ya nchi yake.

Lakini huyu yupo tayari kufa au kuuawa kwa sababu ya pesa tu. mercenary ana tabia ya Kimalaya Malaya tu.

Na tunao Wanasiasa mercenary, ni mercenary. Mtu yoyote anaweza kuwalipa tu, mtu yoyote, anakwambia mapesa haya hapa, utanifanyia kazi

Na tunayo mijitu humu, inafanya kazi si za wananchi hapa ni za watu wengine..hawa ni mercenary.. malaya Malaya tu. Halafu wapumbavu hawa, wanafikiri tunaunda jeshi la mercenary, wendawazimu hawa.

Sasa wamekiona cha mtema kuni. Na tumewatangazia, tumesema waende wapumbavu hawa kama hatujawatia ndani wote hawa. Tumepata aibu mara moja wanafikiri tunaweza kupata aibu mara mbili tena.

Jeshi letu ni jeshi la Wananchi wa Tanzania..sijui hawaelewi!!? Ni jeshi la Wananchi wa Tanzania Sio jeshi la Vibaraka Malaya Malaya eeh?.

Kwahiyo Vijana msijali, Msiwe na wasiwasi hata kidogo. Tunawajua, tutawasaka mmoja mmoja, mmoja mmoja.. Malaya watupu hawa, tutawasaka mmoja mmoja, na kila tutakapo wasaka tutawatangazieni kwamba Malaya mmoja tumeshamshika." Mwisho wa kumnukuu.

Je, unamtizamo gani juu ya haya aliyoyasema kutokana na hizi zama tulizo nazo. Je, wanaohama Wanaunga juhudi za rais au ni mercenary?

VIDEO:

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad