Kafulila Atuma Ujumbe kwa Rais Magufuli


Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia Chama Cha NCCR - Mageuzi na baadaye kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa katibu tawala wa Mkoa wa Songwe amedai anafurahia kufanya kazi na kiongozi huyo wa nchi kwa kile alichokidai amekuwa mtu wa kufanya maamuzi.

 

Kafulila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv ambayo ilitaka kufahamu juu ya ujumbe wake ikiwa ni leo kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Kafulila amesema “ninamuombea kwa Mungu amzidishie maisha marefu na azidi kumjenga kwenye haya anayosimamia, kuna mambo mengi ambayo kipindi chake yeye yanatakelezeka sana, hasa kwenye usafiri wa anga na miundombinu mingine”.

“Kazi yangu ya utendaji hasa zama za Magufuli imekuwa nyepesi kwa mtendaji mwaminifu, na hasa ukiwa mtendaji ambaye hupendi rushwa, mi nafurahia sana nipo kwenye utendaji, ningekuwa kwenye ubunge ningependekeza lakini mimi kama mtendaji ninatakiwa kufanya maamuzi.”Ameongeza Kafulila

Julai 28 mwaka huu Rais Magufuli alitangaza kuwateua baadhi ya makada waliokuwa wamehama kutoka upinzani na kujiunga na CCM kwa nia ya kumuunga mkono, akiwemo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Moses Machali  na David Kafulila kama Katibu Tawala wa Songwe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad