Kagera Sugar Yajifunza Kutokana na Makosa

Kagera Sugar yajifunza kutokana na makosa
Unapoizungumzia Kagera Sugar hivi sasa ni moja kati ya timu ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu, ikiwa sambamba na JKT Tanzania, Azam Fc pamoja na Yanga.


Kagera Sugar pia ni timu ambayo inashika nafasi ya tatu kwa kufunga mabao mengi mpaka sasa katika ligi, ikiwa imeshafunga mabao nane sambamba na Singida United. Mtibwa Sugar na Mbeya City zikiongoza kwa mabao yake 10, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga pamoja na Stand United zenye mabao tisa ya kufunga.

Katika miaka ya karibuni, timu hiyo imekuwa haifanyi vizuri katika ligi kama ilivyozoeleka, hali ambayo imewapelekea kuwa inaponea chupuchupu kushuka daraja katika dakika za mwisho za msimu.

Msimu huu imeanza vizuri mpaka sasa ikiwa katika nafasi ya tisa ya msimamo kwa alama 10, nafasi moja nyuma ya mabingwa watetezi Simba iliyopo katika nafasi ya nane na alama 11.

Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema kuwa wamejifunza kutokana na mwanzo mbaya wa ligi msimu uliopita na watahakikisha wanapambana katika kila mchezo na hatimaye kujiwekea mazingira ya kumaliza katika nafasi nzuri mwishoni mwa msimu.

Kwa hatua inayoendelea kuionesha mpaka sasa katika ligi, huenda klabu hiyo ikamaliza hatua nzuri mwishoni mwa msimu na kurejea katika zama zake ambazo timu hiyo ilikuwa ikifanya vizuri katika ligi na kuleta ushindani kwa vigogo Simba, Yanga na Azam Fc.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad