Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo 17.10.2018 kitafanya kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya chama hicho kitachokuwa na agenda kuu ya kujadili na kuazimia kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya chama kitakachofanyika jijini Dar es Salaam
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.
Muungwana Blog inafahamu kuwa pamoja na mambo mengine Kamati Kuu hiyo imepanga kujadili suala la kuvuja kwa sauti za Wabunge wake, Saed Kubenea wa Ubungo na Anthony Komu wa Moshi Vijijini ambao walisikika wakiongelea suala la ukomo wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.
Leo wakati Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema akizunguma na wanahabari kuhusu kutekwa kwa Bilionea Mohammed Dewji, Muungwana TV ilimuuliza Mkurugenzi wa Mawasiliano, John Mrema iwapo uongozi wa juu wa chama ulisikia sauti zile ambapo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo.