Kambi ya Taifa Stars Tumejipanga Hatujakurupuka -Mwakyembe

Kambi ya Taifa Stars Tumejipanga Hatujakurupuka -Mwakyembe
SERIKALI imesema maandalizi ya Kambi ya Taifa Stars yanaendelea vizuri wala mamlaka hiyo haijakurupuka badala yake imejipanga vyema kuhakikisha kambi inakuwa nzuri na salama kwa amaandalizi hayo dhidi ya Timu ya Taifa ya Lesotho.



Hayo yamethibitioshwa leo Alhamisi, Oktoba 25, 2018 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, dkt. Harrison Mwakyembe na kusema michango ya Watanzania na Taasisi mbalimbali bado inahitajika kwa safari ya Taifa Stars kuweka kuweka kambi nchini Afrika Kusini.



“Tunafuatilia kwa makini Kambi hiyo ya Afrika Kusini hatujaingia kichwa kichwa, tupo makini sana. Wizara yangu, TFF na Wizara ya Mambo ya Nje tunashirikiana kwa ukaribu kuhakikisha kambi nzuri ya Afrika Kusini na salama kuelekea mchezo dhidi ya Lesotho.



‘Tunawashukuru wote waliochangia katika safari ya Cape Verde, bado tunawaomba mchango wao wa hali na mali kuelekea mchezo wa Lesotho TFF na Wizara tunashirikiana kwa kiasi kikubwa kuhakikisha timu inapata maandalizi mazuri ya mchezo huo.



‘Gharama za kuisafirisha Taifa Stars zimeongezeka zaidi ya bajeti ya awali kutokana na kambi ya nje ya nchi (Afrika Kusini), tunazungumza na mashirika ya ndege tupate bei nzuri, pia kampuni za mabasi ili Watanzania wengi waende kuishangilia timu yao,” amesema Waziri Mwakyembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad