Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Bashiru Alli amelipomgeza Jeshi la Polisi nchini kwa kufanikisha kupatikana kwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji maalufu Mo.
Dkt Bashiru ambaye alikuwa nchini China kwa ziara ya siku kumi ya kikazi ameyasema hayo jana baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa na Mwalimu Nyerere na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake.
Alisema jambo la kwanza analipongeza Jeshi hilo la Polisi kwa kumpata Mo Dewji nakwamba taswira ya nchi ingechafuka kama mfanyabiashara huyo asingepatikana.
” Ndugu zangu waandishi mnajuwa kuna baadhi ya watu walishaaza kulopoka na sasa wameumbuka hivyo nalipongeza Jeshi la polisi tena saana.”alisema
Akizungumzia safari yake hiyo ya China Dkt.Bashiru alisema wamekuwepo nchini humo kwa siku kumi na kwakweli wamejifunza mambo mengi na wameweza kukutana na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuja kuweka nchini.
” Kwakweli safari ilikuwa nzuri sana tumezungumza na watanzania ambao wanaishi kule,tumefanya mazungumzo na makampuni mengi takribani 12 madogo kwa makubwa na wamezungumzia suala la kufanya uwekezaji hapa Tanzania.” alisema Dkt Bashiru
Alisema kuwa mkoani Tanga utafanyika uwekezaji mkubwa wa kiwanda,pamoja na Bagamoyo na makampuni haya yalianza kufanya mazungumzo na Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa nchini humo kwa ziara ya kikazi hivyo wanakuja .
Dkt.Bashiru alisema wamejifunza mambo mengi mno na kipekee wamejifunza mambo manne makubwa ambayo moja ni kujenga muafaka na mwelekeo wa nchi yao kwani kwao katika hilo si mjadala tena na hakuna siasa.
Pia pamoja na kuendelea kwao lakini bado wamejiweka katika nchi ambayo inaendelea na wanamfumo mzuri wa kuzalisha vijana nakuwapa mafunzo ambayo kimsingi si hiari ni lazima.
Dkt. Bashiru amesema kwa namna utaratibu au mfumo ambao wamejiwekea ni kwamba hakuna ambacho kinaweza kufanyalika pasipokujadiliana kwa pamoja .
Alimaliza kwakusema kuwa wachina wamewekeza kwa mgawanyo kwa maana katika sekta ya afya,elimu … Lakini kubwa wamezungumza na makampuni hayo makubwa nakwamba wachina wako mbali .
Hata hivyo Dkt Bashiru amewataka waandishi wa habari kusaidia kukuza uchumi wa nchi kwa kuhabarisha jamii.mambo ambayo yanafanywa na jitihada zinazofanywa na watendaji.