Kauli ya Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya nje Baada ya Kuapishwa Leo na Rais Magufuli

Kauli ya Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya nje Baada ya Kuapishwa Leo na Rais Magufuli
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Faraji Mnyepe amesema watendaji katika wizara hiyo wamezoea kufanya kazi kwa mazoea kuwa kituo cha kufanyia kazi ni nje ya nchi.

Dk. Mnyepe amesema hayo leo Jumatano Oktoba 3, Ikulu jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, kuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo.

“Nikutoe hofu Mheshimiwa Rais, nakwenda kufanya kazi sina wasiwasi na idhini yako uliyonipa nikafanye kazi. Nilisikia ulipomuapisha Naibu Waziri (Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro) ulisema wazi wizara hiyo haifuraishi.

“Ulitoa sababu na sababu zile ni za kweli zote. Matatizo ya wizara yako mengi lakini katika salamu zangu hizi naomba niyakweke katika sehemu mbili, ya kwanza barua kwa nini hazijibiwi.

“Mentality (dhana) au culture (utamaduni) ni kwamba ukishaajiriwa katika wizara ile kituo chako cha kazi ni nje ya nchi, kwa hiyo mtu ukishateuliwa ukirudishwa unarudishwa ili utafutiwe kituo kingine cha kazi, hiyo ndiyo mentality.

“Kuna makundi katika wizara ile kama ulivyoanisha siku ile, mengi sana… Mheshimiwa rais naenda kuishi katika kiapo changu,” amesema Dk. Mnyepe.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pia mh raisi magufuli shughulikia ofisi za ubalozi wa tz ughaibuni. Customer service ni mbovu hasa UK yule Dada ashughulikiae mambo ya uhamiaji. Ni mkali mno, hataki kuulizwa hadi unamwogopa, anataka kunyenyekewa km ilivyokuwa tz ya zamani kabla ya magufuli. Pia kuna mtu wamemweka si wa tz, lolote unalomuuliza hana jibu. Kazi yake ni kukuambia upige baadae. Sauti yake si ya mzungu ni mwanaume. Kwa kweli km una shida ni vigumu kupata huduma ya kuridhisha kwa njia ya simu ubalozini wa tz nchini UK. Wapo watz wengi wasomi wanahangaika na ajira na wanajua kiswahili na kiingereza, kwanini wamweke huyo mwanaume ambaye kiswahili hajui na kiingereza ni lugha ya kujifunza. Mh rais tafadhali fanya review ubalozi wa tz uko UK.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad