Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kenya inachunguza uhalali wa aliyekuwa Rais wa tafa hilo, Mwai Kibaki kutumia madaraka yake kutoa ufadhili huo
Akiwa mbele ya kamati hiyo aliyekuwa Mkuu wa Huduma za Umma, Francis Muthaura ametetea kitendo hicho cha Kibaki
Amesema kuwa Kibaki alikuwa akijaribu kuwasaidia Watoto wa ndugu yake, Philip Githinji aliyepoteza kazi katika Kampuni ya Oil Libya
Vijana hao Ian Nderitu na Sandra Njeri walipelekwa kusoma fani ya Uhandisi na Usinifu Majengo katika Taasisi ya Teknolojia ya Royal Melbourne nchini Australia
Kamati hiyo ya Bunge imesema kuwa ufadhili huo ulikuwa mkubwa sana kwakuwa wawili hao waliendelea na Shahada ya Uzamili baada ya kumaliza Shahada yao ya kwanza
Mbunge, Otiende Amollo amesema kuwa kiongozi akitaka kuwasaidia nduguze anapaswa kutumia fedha zake na si za umma