Kigogo Mwingine wa Migodi Mikubwa Nchini Kortini Kwa Kutakatisha Pesa


Mkurugenzi  mtendaji  migodi wa Pangea, North Mara na Bulyanhulu, ASA Mbulaja Mwaipopo, leo Novemba 23.2018 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka tisa likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni Tisa.

Mshtakiwa Mwaipopo ambaye pia ni mhandisi wa madini amesomewa mashtaka yake jana mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja  Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Mutalemwa Kishenyi na Jackilline Nyantori.

Mbali na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yako manne, Mwaipopo pia anashtakiwa na shtaka moja la kula njama, shtaka moja la kuongoza kutendeka kwa uhalifu, shtaka moja la kughushi, mashtaka mawili ya kukwepa kodi.

Mshtakiwa Mwaipopo anatarajiwa kuunganishwa na washtakiwa wenzake ambao ni Rais wa zamani wa migodi hiyo,  Deogratias Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo ambao mwisho mwa wiki iliyopita  (Oktoba 17.2018) walisomewa mashtaka 39, yakiwemo hayo Tisa aliyosomewa Mwaipopo jana, yakiwemo pia ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya USD milioni 112.

Mbali na Mwanyika, Lugendo na Mwaipopo washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya Mwaipopo wakili Nchimbi alidai, washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11.2008 na June 30.2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.

Imedaiwa katika kipindi hicho na mahali hapo Mwaipopo na wenzake, pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya ya kutenda makosa ya kughushi na ukwepaji wa Kodi.

Pia mshtakiwa anadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

 Aidha mshtakiwa Mwaipopo na wenzake,wadaiwa kati ya Mei 16.2008 na Desemba 31,2008 huko Kahama na Biaramulo, walitoa tamko la uongo kwa kamishna Generali wa  TRA kwa nia ya kukwepa kodi kulipa USD 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

Katika shtaka la kughushi washtakiwa hao wakiwa na nia ya ulaghai waligushi mkataba wa mkopo wakitaka kuonyesha kwamba Aprili 30.2014 Kampuni ya Pangea limited ilikubali kukopa USD 90,000,000 ikiwa na riba Kutoka benki ya kimataifa ya barrick huku wakijua kuwa siyo kweli.

 Hata hivyo wa mshtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na kesi itatajwa tena oktoba 31, mwaka huu ambao Mshtakiwa Mwaipopo ataunganishwa na wenzake
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad