Kimenuka ''Wamiliki Ardhi Airport Kufutiwa Hatimiliki''


Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), kufuatilia na kufuta hati za umiliki wa ardhi za kampuni zilizopo Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Kambarage nyerere (JNIA).


Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye wa kwanza kulia.

Akizungumza leo katika ziara yake alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Nditiye amesema haiwezekani kwa kampuni binafsi za Puma Energy na Tanzan air kuwa na hati za kumiliki ardhi katikati ya uwanja wa ndege wa Serikali.

"Hati hizi zinapaswa kufutwa haraka sana na hizi kampuni nilizozitaja zinapaswa kupangishwa katika uwanja huo, kuna madhara makubwa mtu binafsi kuwa na hati katikati ya uwanja." amesema Nditiye.

Nditiye amesema TAA inapaswa kuhakikisha inalifikisha suala hilo wizara ya ardhi na taasisi nyingine za Serikali ili hati hizo zifutwe na kukabidhi maeneo hayo kwa serikali ndani ya muda utakaopangwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad