Kishoka Tanesco Achukua Tsh Milion 24.6 Kwa Wananchi


Mkandarasi hewa wa Shirika la Umeme nchini(TANESCO), aliyejulikana kwa jina moja la Kileo anadaiwa kukusanya fedha hizo kutoka kwa Wananchi 22 wa Kijiji cha Manyire-Mlangarini, Arumeru mkoani Arusha kama gharama ya kuwaunganishia nguzo 40 za umeme

Afisa Usalama TANESCO Mkoani humo, Frank Shida amesema hayo yamebainika katika operesheni iliyolenga kukamata wateja haramu waliojiunganishia umeme kupitia vishoka

Amesema mchanganuo wa fedha hizo ni Tsh. 861,000 gharama ya nguzo kwa kila mtu, Tsh. 40,000 za fomu kila mtu, kuchimba mashimo Tsh.15,000 kila mtu na Tsh. Milioni 4.5 kutoka kwa Joramu Muganda na kufanya jumla ya Tsh. 24,652,000

Alifafanua pia kuwa Kijiji hicho kina nguzo zaidi ya 40 ambazo si mali ya shirika ila waya uliotumika ni mali ya TANESCO lakini laini ya waya uliotumiwa ni ndogo kwa aina ya nguzo walizoweka

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad