Kocha Yanga Amponda Diamond Platinum

Kocha Yanga Amponda Diamond Platinum
Si kwenye soka pekee hata kwenye muziki yumo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa huwa hapendi kusikiliza ny­imbo za msanii wa Bongo Fleva, Diamond Plat­numz sababu ni mjanjamjanja.

Kocha huyo am­baye ni raia wa DR Congo na Ufaransa ambako muziki ndiyo nyumbani kwake, amekuwa akifuatilia muziki wa hapa nyumbani lakini amevutiwa zaidi na AliKiba.

Kwa mujibu wa Championi Juma­tano, kocha huyo alisema muziki wa hapa Bongo ame­kuwa akiufuatilia ingawa sio sana kama ulivyo wa kwao Congo.

“Muziki wa hapa ndiyo ninaufuatilia kwa kiasi fulani, na­jua kuna Diamond ila simpendi sana kwa sababu yeye ni mjanjamjanja kwenye mambo yake lakini napenda muziki unaoimbwa na AliKiba.

“AliKiba ni mwanamziki mzuri na muda mwingi nasikiliza muziki ule wa kwetu Congo na kufanya mambo yangu mengine ya soka,” alisema Zahera.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad