Kumbe Tupac Yuko Hai Aonekana Nchini Malaysia

Kumbe Tupac Yuko Hai Aonekana Nchini Malaysia
Story kubwa ambayo inatrend kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu  Tupac Shakur kudaiwa kuwa hai na kuonekana akiwa nchini Malaysia, mtoto wa mtayarishaji wa muziki Sude Knight ametumia ukurasa wake wa instagram kuthibitisha hilo.

Suge J Knight ameweka picha pamoja na videos kwenye ukurasa wake wa instagram kuwathibitishia mashabiki kuwa Tupac yupo hai na kwa sasa anaishi Malaysia na siku si nyingi ukweli utafahamika kuhusu maisha mapya ya Tupac na kudai kuwa amefichwa.



Suge J Knight amepost picha ya Tupac na kudos ndio muonekano wake wa sasa akiwa nchini Malaysia na kuandika “Wamewadanganya kwa mara ya kwanza lakini amekuwa hai” na akaongezea video ikimuonyesha Tupac na kusema “Video ya hivi karibuni kutoka Malaysia”.

Marion Knigt Jr maarufu kama Suge alikuwa CEO wa Death Row Records studio ambayo ilikuwa ikifanya kazi za Tupac Shakur na hivi karibuni amehukumiwa kifungo cha miaka 28 jela kwa kukutwa na hatia ya kugonga na kuua. Suge alikuwa na Tupac kipindi anapigwa risasi September 7 ,1996.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad