Lema Atema Cheche Kutekwa kwa Mo Dewji Aitaka Serikali Ikubali Vyombo vya Nje Kuchunguza

Lema Atema Cheche Kutekwa kwa Mo Dewji Aitaka Serikali Ikubali Vyombo vya Nje Kuchunguza
Mbunge wa Arusha mjini ambaye ni waziri kivuli wa mambo ya ndani Godbless Lema ameitaka serikali kuruhusu vyombo vya kimataifa kufanya uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji.

 Lema ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 16, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa hiyo ndio njia pekee ya Serikali kujiondoa katika lawama.

Amesema kutokana na hali halisi ya eneo alilotekwa Mo Dewji ulinzi ulivyokuwa mkubwa na CCTV za kutosha kutokjana na maeneo wanaokaa viongozi wakubwa anashangazwa ni kwanini adi sasa Mo ajapatikana.

Pia amemtaka waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola Kuacha Kuwazuia watu kujadiri tukio hilo na kuwataka washauri wa raisi wamshauri vizuri ili aweze kukubali kuleta wapelelezi wa nje ili kuchunguza tukio la Mo na matukio ya utekwaji yaliyowahi kufanyika nyuma.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad