Mbunge wa Chadema Arusha Mjini, Godbless Lema, mbaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, amesema, leo atazungumza na waandishi kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji.
Amesema mkutano huo na waandishi utafanyika makao makuu ya Chadema mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Katika Twitter Lema aliiandika jana ikisema, “Nafikiri kwa sasa ninaweza kuongea na waandishi wa habari kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji.”
Posti ya Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa twitter jana ipo hapa chini.
Lema Kuzungumza na Waandishi wa Habari Kuhusu Kutekwa kwa Mo Dewji
0
October 16, 2018
Tags