Liverpool kuitumia Cardiff City kama ngazi

Liverpool kuitumia Cardiff City kama ngazi
Klabu ya Liverpool inashuka dimbani jioni ya leo kukipiga na Cardiff City katika mchezo wa ligi kuu ya England ambao utarushwa na East Africa Television kuanzia saa 10:30 jioni, lakini mchezo huo unaweza kuwapaisha Liverpool kileleni.

Liverpool ambao wana alama 23 katika nafasi ya pili wakishinda leo wataondoa kileleni mwa msimamo vinara Manchester City ambao nao wana alama 23 lakini wanaongoza kutokana na kuwa na wastani mzuri wa ambao ya kufunga na kufungwa.

Cardiff City huenda ikawa ngazi ya Liverpool kupanda kileleni kutokana na mwenendo wa timu hiyo ambayo imerejea ligi kuu msimu kutokuwa mzuri ambapo hadi sasa imeshinda mechi 1 tu kati ya 9 ilizocheza.

Katika mechi hizo Cardiff City imefungwa mechi 5 na kutoa sare 2 ambazo zimewafanya kuwa na alama 17 wakiwa katika nafasi ya 17.

Safu ya ushambuliaji ya Cardiff City pia sio nzuri kwani ina uhaba mkubwa wa mabao ambapo hadi sasa mchezaji mwenye mabao mengi ni Josh Murphy ambaye amefunga mabao mawili huku mchezaji aliyetoa msaada mara nyingi ni Sean Morrison akiwa nazo mbili.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad