Lowassa: Nchi Inajengwa Hofu na Chuki

Lowassa: Nchi Inajengwa Hofu na Chuki
WAZIRI Mkuu wa Zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, Edward ngoyai Lowassa amedai kuwa kwa maoni yake anaona nchini kuna tatizo la hofu na chuki mingoni mwa wananchi.



Lowassa ameyasema hayo leo Ijumaa, Oktoba 12, 2018 wakati wa Mdahalo wa Wazi wa Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasomi, wanasiasa, wanazuoni na wataalam wa masuala ya siasa kutoka ndani na nje ya nchi.



“Mimi naona nchini inajengwa hofu kubwa sana kwa wananchi wakati wa uchaguzi, hofu hii inawafanya wachague watu ambao hawakupenda kuwachagua, pale Monduli tulifanya uchaguzi, kale kamji kadogo kulikuwa na Landrover za polisi 45 na magari ya upupu 4 utafikiria kuna vita, lakini vitu hivyo ndivyo vinavyofanywa kwa kutumia vyombo vya dola kusimamia uchaguzi.



“Chuki inakuwa mbaya sana ukiwa mwanachama wa CCM na mwenzako ni CHADEMA basi mchukiane na hii inatia hofu watu, nchi imekuwa na amani na utulivu kwa miaka mingi sana tukiona mambo haya yanatokea ni lazima tuyachukulie hatua. Pengine katiba ile ya warioba kama wanasiasa wangekubali kushirikiana, katiba inamapendekezo ya wazee ambao wanaweza kuwaita viongozi wakawaambia hili
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad