Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku amefunguka juu ya matamanio yake ya kucheza ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A ndani ya timu ya Juventus akidai kuwa wanamipango kabambe kwenye soka.
Mbelgiji huyo amecheza mechi 10 kati ya 11 ndani ya United msimu huu nakufanikiwa kufunga mabao manne huku akiifungia magoli 45 timu kwenye timu yake ya taifa yakiwemo dhidi ya Switzerland waliyo ibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-1 siku ya Ijumaa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa wa miaka mitano unafikia tamati mwaka 2022 ndani ya Old Trafford alipojiunga akitokea Everton.
Wakati alipoulizwa kuhusu hatma yake ya baadae, Lukaku amesema kuwa anaelekea Italia huku akisisitiza kwa nini ishindikane lazima itatokea.
“Juve wanamipango kabambe katika soka na ambayo endelevu, kila mwaka wanazidi kuimarika. Pasipo shaka, Juve ni miongoni mwa timu bora zaidi kati ya mbili au tatu barani Ulaya,” amesema Lukaku.
”Wana kocha bora na kila idara wanawachezaji wenye kiwango cha hali ya juu. Cristiano Ronaldo yupo nje lakini hebu watazame hawa wengine, Paulo Dybala anavutia na anazidi kuimarika lakini pia namkubali Douglas Costa.”
Nakusema Juventus ni moja ya klabu kubwa barani Ulaya, wakati United itakuwa mwenyeji mbele ya vibibi hivyo vya Turin mwezi Novemba michuano ya Champions League hatua ya makundi.