Mabasi ya Mikoani Kuanza Safari Saa 11 Alfajiri Kuanzia Wiki Ijayo

Mabasi ya Mikoani Kuanza Safari Saa 11 Alfajiri Kuanzia Wiki Ijayo
Serikali imetanga kuanza mpango wa mabasi ya abiria katika mikoa mitano nchini, kuanza safari za ndani na nje ya nchi saa 11 alfajiri kuanzia Oktoba 9, 2018 ili kurahisisha safari kwa abiria na kufika mapema.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari  Oktoba 4,  2018 jijini Arusha, katika ziara ambayo aliifanya Uwanja wa Ndege wa Arusha, alisema awali safari hizo, zilitarajiwa kuanza mapema lakini kuna masuala yaliyokuwa yanashughulikiwa na Sumatra.

"Kuanzia Jumanne ijayo, Oktoba 9, baadhi ya magari ya abiria katika mikoa mitano, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma yataanza safari saa 11 alfajiri," alisema.

Alisema alitoa agizo hilo kwa mara ya kwanza, akiwa Ubungo jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita lakini safari hizo zilichelewa kuanza kutokana na Sumatra kuwasiliana na vyombo vingine ikiwepo polisi na wamiliki wa mabasi ili kurekebisha ratiba.

Naibu waziri huyo, amesema hatua hiyo pia itachukuliwa kwa mikoa mingine, baada ya kujiridhisha kuwa kutakuwa na usalama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad