Mahakama yatoa amri ya kukamatwa kwa Mfanyabiashara Ndama Mtoto Ya Ng'ombe


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kukamatwa kwa Mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein baada ya kukiuka taratibu za dhamana 

Pia, Mahakama hiyo imetoa barua ya wito kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo kufika Mahakamani hapo 

Hakimu Maira Kasonde ametoa hati hiyo leo baada ya Ndama kushindwa kufika Mahakamani ili akajieleze kwanini asifutiwe dhamana yake 

Kabla ya kutolewa kwa amri hiyo, Wakili wa Jamhuri Mosia Kaima amedai hawana taarifa yoyote kuhusiana na mshtakiwa huyo 

Ndama anakabiliwa na mashtaka 5 yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, baada ya kukikri shtaka la 6 la kutakatisha fedha na kulilipia faini
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad