Mama Diamond Ana Ujauzito wa Mtoto wa Tatu


Mama Diamond alithibitisha kuwa mjamzito kupitia mahojiano na anatarajia mtoto wake wa tatu licha ya kuandika mtandaoni ujauzito wake

Sandra Kasim aliwahi kusutwa sana kwa kuingia uhusiano na mvulana mchanga lakini alikanusha madai hayo na kusema Rally Jones ni mtu mzima na kwamba kwake umri haumjalishi

Mama mzazi wa mwanamuziki nguli nchini Tanzania, Diamond Platnumz, Sandra Kasim ameachia picha mtandaoni na kuwaacha watu vinywa wazi kwa mshangao baada ya kuibuka madai ni mjamzito.

Akihojiwa na kituo kimoja jijini Dar es Salaam, Sandra alithibitisha kuwa mjamzito na kwamba baba ya mtoto wake nambari tatu ni Rally Jones.

Mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sandra Kassim ambaye anadaiwa kuwa na ujauzito wa mume wake mwenye umri mdogo. Picha: UGC

“Diamond atapata mdogo wake…basi subirieni mdogo wake wa mwisho,” Sandra alisema.

Baada ya uhusiano wake na Jones kuwa wazi, mama huyo wa watoto wawili alisutwa sana baada ya wengi kudai alikuwa akiiga vitendo vya Zari Hassan na kumkimbilia mchumba wa umri mdogo.

Lakini Mama Diamond alijitokeza na kukanusha madai hayo na kusema, Jones si mtoto mdogo na kwamba yeye hajali kuhusu umri katika uhusiano wake wa kimapenzi.


“Nimeolewa… Ana udongo gani? Angekua mdogo singeona. Ni mkubwa,” alisema.

Mapema mwaka huu, Jones alizua kimbunga mtandaoni kwa kumwita mama ya msanii huyo ‘mke’ wangu na kufanya watu kuhisi wawili hao walifanya harusi ya siri.

Alichapisha picha akiwa amemshika Sandra mkono na kusema kuwa, uhusiano wao ulikuwa ikiendelea vizuri sana.


''Nahisi furaha sana nina mwanamke spesheli kando yangu. Mungu na akupe maisha marefu Inshallah. Happy Birthday mke wangu Mama Dangote. Nakupenda,'' aliandika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad