Manchester United wamwambia Zidane asubiri, Neymar amshawishi Pogba


MABOSI wa Manchester United wamemshauri Zinedine Zidane kutotafuta umeneja kwingine wakati wakiamua hatma ya kocha wa sasa wa miamb hiyo ya England, Jose Mourinho. (Mirror) 

Mashabiki wa United walipigwa picha na bango la picha ya meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zinade, 46 nje ya Old Trafford kabla ya ushindi wa siku ya Jumamosi dhidi ya Newcastle. (Eurosport) 

Machester United watahitajika kumlipa Mourinho pauni milioni 29 ikiwa watamfuta meneja huyo  lakini kiwango hicho kitashuka hadi paunia milioni 10 ikiwa atamaliza msimu na United washindwe kumaliza katika nafasi za Ligi ya Mabingwa. (Mirror) 

Mourinho alifichua kuwa alipokea ujumbe wa imani naye kutoka bodi ya Manchester United kabla ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle. (Times - subscription required) 

Tanguy Ndombele 
Manchester City watahitajika kuvunja rekodi yao ya kusaini wachezaji kwa kumsaini kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele baada ya klabu hiyo ya ufaransa kumwekea thamani ya pauni milion 70 mchezaji huyo wa miaka 21 mwezi Januari. (Star) 

Manchester United wamemuambia Paul Pogba kuwa hatauzwa mwezi Januari licha ya mfaransa huyo kuripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na Barcelona baada ya wao kuonyeha nia ya kumsaini. (Mail) 

Mousa Dembele 
Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele, 31, hatarajiwi kujadili mkataba mpya na huenda akaondoka wakati mkataba wake utapokwisha msimu wa joto akitarajia kuhamia China au mashariki ya Kati. (Sun) 

Neymar 
Mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris St-Germain na timu ya taifa ya Brazil Neymar amefanya mazungumzo na kiungo wa Manchester United Paul Pogba kumshawishi kujiunga na mabingwa hao wa League 1 baada ya kutokua na mustakabali mzuri wa baadae kwa kiungo huyu mwenye miaka 25. (Goal) 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad