Maskini Rich Mavoko....Nyimbo Alizotoa Baada ya Kutoka WCB Zaonesha Kushuka Kimuziki

Tangu ang'atuke WCB chama kubwa linaloshikilia muziki wa bongo kwa sasa(kubali au kataa huo ndo ukweli) kijana Mavoko anaonyesha jitihada za kuzaliwa upya kisanaa lakini changamoto kubwa naona kama mashabiki wa muziki bongo wamemtupa na kumpuuza kijana wao licha ya kuachia ngoma mbili ndani ya muda mfupi "Ndegere" na "Naogopa" ukisikiliza audio za hizi ngoma dizaini kama kashuka kidogo hasa kwenye wimbo mpya aloachia sept 27 "Naogopa",hadi sasa huko U tube ana views Laki 4 huku Navy Kenzo ambao nao wameachia ngoma yao siku hiyo hiyo wana views zaidi ya Milion 1

Mavoko anatakiwa atulie,ajipange aache papara, lazma afanye mambo makubwa kuprove ulimwengu kwamba huko WCB alikuwa anabaniwa,ila kama ataenda na mwendo huu,ataendelea kuwachukia wenzake bila sababu na kuuona muziki mgumu.

Hivi sasa yuko kwenye media tour ya kuupa promo wimbo wake mpya kashafanya intavyuu kwenye EA radio na Magic but hakuna attention yoyote anayopewa(inauma sana) na mpaka sasa tayari wimbo wake umeshafunikwa na "Katika" wa Navy Kenzo ambao wamemshirikisha Bosi wake

Kuna ule msemo wanasema usiache kazi kabla hujapata kazi, alichokosea Mavoko amejilipua WCB huku hajaandaa mazingira mazuri maisha yake ya muziki baada ya WCB. Ukweli kwa sasa himaya powerful za muziki bongo ni WCB na CMG, kama ukikwazana na mmojawapo hakikisha mwingine umemshikilia vyema, sasa huyu Mavoko naona hata hakujiandaa kupokelewa na upande wa pili, angekuwa ameandaa mazingira tungesikia anavyopigiwa promo la kufa mtu na CMG kwa ajili ya Fiesta kama ilivyokuwa kwa Alikiba na angerudi kwa kishindo kwenye game. Kwa sasa inaonesha ametoswa na pande zote, so sitarajii kama anaweza fika popote, kwa mtazamo wa harakaharaka naona kabisa career yake is over...any way ngoja tumpe muda

By Chinga one/JF

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad