Mastaa Punguzeni Kudanga Muige Mfano Wa Lulu- Sabby Angel

Mastaa Wapunguze Kudanga Waige Mfano Wa Lulu- Sabby Angel
Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Bongo Movie Sabrina Omary maarufu kama Sabby Angel amefunguka na kusema anamkubali sana Lulu na ni mfano wa kuigwa na kuwataka mastaa waige mfano wa Lulu.

Kuanzia Siku ya Jumapili Lulu ametawala headlines zote baada ya kuvalishwa pete ya uchumba  na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye ni CEO wa EFM, Majizzo.

Sabby Angel  amefunguka na kumpongeza Lulu kwa jambo alilofanya kwani badala ya kudanga na kuhangaika ametulia na mwanaume mmoja na sasa wapo mbioni kufunga ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sabby Angel ameandika:

Nimefurahi sana Tena sana kuamka na kuona picha za posa ya Lulu, For real am so happy anaonyesha mwenendo mwema yaani she is a role model. Mwanamke lazima stara. Mastaa wengine wafuate Mfano. Sio kudanga tu na kiki. Kuwa kioo cha jamii lazima uwe Mfano kwani mabinti wengi wadogo hutangalia sisi na kufuata tunayofanya”.

Sabby Angel ametengeneza headlines baada ya kuolewa ndoa yake ya tano baada ya Kuachika mara nne tayari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad