Mauaji ya Mrembo Kenya Utata Mtupu...Mtangazaji wa Television ya CITIZEN Akamatwa

Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari Kenya vimegubikwa kwa kesi inayomhusu mwandishi wa kituo kimoja mashuhuri cha televisheni Kenya, Jackie Maribe.

Jacque Maribe, mtangazaji wa televisheni ya Citizen, amekuwa kizuizini pamoja na mchumba wake aliyekamatwa kama mshukiwa wa mauaji ya mwanamke mmoja mjini Nairobi.

Ni kesi inayozungumziwa pakubwa baada ya kuuawa kwa mwanamke mmoja kwa jina Monica Kimani, na kikubwa ni namna ufichuzi unavyojitokeza katika uchunguzi wa kesi hii.

Na kesi hii imeonekana kuwagusa wengi kwasababu kumeshuhudiwa msururu wa mauaji ya kinyama nchini.

Mapema mwezi huu Sharon Otieno mwanafunzi wa chuo kikuu aliyekuwa mja mzito aliuawa kwa kudungwa kisu. Na kufuatia sasa na kesi ya mauaji ya Monica Kimani aliyeuawa nyumbani mwake.

Suali kubwa linalojadiliwa ni nini kinachangia mauaji kama haya na vipi yanavyoweza kudhibitiwa?

Wakenya wanafuatilia kwa makini namna polisi na upande wa mashtaka wanavyozishughulikia kesi hizi, katika mfumo wa sheria ambapo vitendawili vya baadhi ya kesi za mauaji vimeshindwa kuteguliwa, na kuishia kusalia wazi hadi ushahidi mpya utakapo patikana.
Mambo makuu kuhusu kesi hii ni yapi?

Mauaji ya Monica:
Monica Kimani mwanamke mwenye umri wa miaka 29, alipatikana akiwa ameuawa kikatili ndani ya chumba chake wiki iliyopita katika mji mkuu Nairobi.

Monica alipatikana nyumbani mwake siku ya Alhamisi inaarifiwa muda mfupi baada ya kuwasili nchini kutoka Sudan kusini.

Kakake Monica aliugundua mwili wa merehemu dada yake ndani ya bafu baada ya kushindwa kumpata kwenye simu tangu jana yake.

Alikuwa amekatwa shingo na mwili wake ulikuwa ndani ya bafu.




Kukamatwa kwa Jowie:
Taarifa zilichipuka baada ya hapo za kukamatwa kwa mshukiwa aliyekuwa na jeraha la kupigwa risasi begani.

Joseph Irungu anayefahamika kwa umaarufu 'Jowie' anaarifiwa kwenda katika hospitali moja Nairobi kutafuta matibabu na baadaye akaruhusiwa kwenda nyumbani.

Taarifa aliyotoa haikuwiana na matukio.

Alifananishwa na picha zilizonaswa kwenye kamera ya cctv katika makaazi ya Monica kuwa watu walioonekana mwisho kumtembela marehemu.

Kinachofahamika kufikia sasa kumhusu Jowie ni kwamba yeye ni mlinzi binafsi wa kuajiriwa, anafanya kazi katika nchi za kiarabu kama mlinzi wa kibinfasi kwa watu mashuhuri.

Kesi dhidi ya Maribe:
Jackie Maribe, alihojiwa na maafisa wa idara ya upelelezi, kusaidizi kubaini masuala yaliojitokeza katika taarifa aliyorekodi mchumba wake Jowie na wengineo waliohojiwa katika kesi hiyo.

Baada ya hapo taarifa zilichomoza kwamba amekamatwa .

Mwanahabari Jackie Maribe alikamatwa Jumamosi kufuatia agizo lililotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelzi George Kinoti.

Kinoti alisema''Inaonekana alikuwa na ufahamu kuhusiana na haya yote lakini kile anachofanya ni kuficha ukweli kumkinga mshukiwa. Hatujui kwa nini''

Akielezea zaidi sababu za kuagiza mwanahabari huyo akamatwe, Kinoti alisema ni hatia kuficha ukweli kuhusu mauaji na mtu anaweza kushtakiwa kwa ukweli ukibainishwa.

Hii leo mbele ya mahakama, Jackie Maribe ameagizwa kuendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri jijini Nairobi kwa siku 11, kama mshukiwa katika kesi ya mauaji ya Monica Kimani ili kupatia upande wa mashtaka muda wa kukamilisha uchunguzi.

Wakili wake Katwa Kigen, amesema kuwa sababu zilizotolewa na upande wa mashtaka hazikuwa na na uzito unaostahili.

Bwana Kigen pia amaesema mazingira aliyozuiliwa mteja wake wikendi iliyopita hayakuwa mazuri akiongeza kuwa Maribe alidhalilishwa na kuzomewa na mahabusu wenzake.

Wakili huyo pia ameomba mahakama kumhakikishia kuwa haki ya mteja wake Kamba mshukiwa hazitakiukwa.
Katika umuzi wake hakimu, Justus Kituku ameagiza polisi kumhakikishia usalama Bi Maribe akiwa seli akiangazia mfano wa kisa cha hivi maajuzi ambapo mshukiwa wa jaribio la mauaji dhidi ya afisa wa serikali alifariki akiwa kizuizini katika mazingira ya kutatanisha.

Mahakama pia ameamuru mshukiwa asilazimishwe kuandikisha taarifa bila kuwepo kwa wakili wake.

Kwa nini waziri huyu anataka ng’ombe wawe na wizara
Mingoni mwa wale waliyokua mahakamani ni wazazi wake Maribe, Bwana na bi Mwangi ambao walishindwa kuhimili uchungu wa kumuona mwana wao akiondolewa katika ukumbi wa mahakama chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Shughuli ya uchunguzi inaendelea

Polisi wanachunguza ikiwa jeraha la risasi katika bega la mshukiwa mkuu, Joseph Kuria Irungu ni la kujipiga mwenyewe baada ya kutilia shaka madai ya awali kwamba alipigwa risasi na watu wasiojulikana.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Irungu huenda alijaribu kujitoa uhai kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya nyumba ya Maribe Septemba 20.
Bunduki hiyo inaendelea kuchunguzwa ili kubaini iwapo ndiyo iliyotumika kumpiga risasi Irungu begani.
Irungu na Maribe walikuwa wamewambia polisi kwamba walishambuliwa ndani ya nyumba yao lakini baadae wakabadilisha taarifa hiyo na kusema kuwa walishambuliwa nje ya nyumba yao.
Aidha maafisa wa upelelezi walipata nguo, zilizoraruka nyuma ya nyumba ya Maribe, ambazo vile vile zinafanyiwa uchunguzi kubaini iwapo ndizo alizokuwa amevalia Irungu siku anapodaiwa kutekeleza mauaji hayo.
Maafisa hao pia wamechukuwa alama za vidole kutoka kwa gari la mtangazaji huyo ambalo linadaiwa kutumiwa na mpenzi wake Joseph Irungu.
Hii ni kesi ya pili kubwa inayohusisha kukamtwa kwa watu mtu mashuhuri Kenya katika wiki kadhaa iliyozusha minong'ono katika mitandao ya kijamii nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad