Mavoko ajibu kauli ya Sallam kwamba bado anadaiwa na WCB ‘tuheshimiane


Msanii wa muziki kutoka label ya Bilionea Kid, Rich Makovo amefunguka kwa mara ya kwanza toka aachane na uongozi wa WCB.

Muimbaji huyo alikuwa kimya  kutokana na mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa mtandaoni kwamba alikuwa ananyonywa na label hiyo kubwa ya muziki kwa sasa nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Akizijibu tuhuma alizozitoa mmoja kati ya mameneja wa WCB, Sallam kwamba msanii huyo bado anadaiwa na WCB kutokana na uwekezaji uliofanywa, Mavoko amedai kila mtu anatakiwa  ku mheshimu mwenzake huku akisisitiza huu sio muda wa kuanza kueleza nani alimkosea mwenzake.

“Unajua kwenye masuala ya kumzungumzia Rich Mavoko unazungumzia brand ambayo ilikuwepo,” alisema Mavoko “Kwahiyo uliichukua unataka kufanya nayo biashara, sasa unasema hajarudisha na huyo mwenye talent atakuwa amepata. Mimi sitaki kuongelea sana hivi vitu kwa undani, kila mtu anatakiwa kuheshimu kitu cha mwenzake kwanza halafu tuanze kuongeleana na kwenye kuongeleana vitu vibaya ni kutaka mtu kijitetea,”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad