Mbunge Aliyejiuzulu CHADEMA Akana Kuandikiwa Barua

Mbunge aliyejiuzulu CHADEMA akana kuandikiwa barua
Aliyekuwa Mbunge wa Babati mjini, Pauline Gekul amejibu madai ya makada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wanaomshutumu kuandikiwa barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kutokana na barua hiyo kuwa na kasoro na kufanana na barua zingine za wabunge waliojiuzulu kabla yake.

Akijibu madai hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv, Gekui amesema, “wanadamu wakiamua kutafuta makosa kwako hawayakosi, utakuwa mtu wa ajabu unayeangalia zaidi maandishi badala ya ujumbe wa barua, uandishi wa barua mimi siangalii, kwangu sikuona kama ni hoja.”

“Hizo content (ujumbe) ni za kwangu haijalishi imeandikwa na nani kama ni msaidizi wangu au mimi mwenyewe tuangalie ujumbe. Haijalishi kama umeandika barua kwa lugha gani iwe kiarabu, kifipa au kingereza mwisho wa siku watu wanahitaji maana ya ujumbe uliouandika kwa hiyo mi naomba wahangaike kujibu hoja zangu”, ameongeza Gekui.

Hivi karibuni  katika mtandao wa Twitter Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene alikosoa uandishi wa barua za wabunge waliojiuzulu kwa kuandika,

“Kati ya vitu vya hovyo, kijinga, vinavyodharaulisha, kutweza; heshima, uwezo, hadhi na uhalali wao katika jamii, wanavyofanyiwa hawa watu ni hili la kuandikiwa barua, ambayo ni mojawapo ya dalili za kuhongwa. Ukishakuwa corrupted (mla rushwa) hauwezi ku-determine terms(kutambua maneno). Unakuwa msahibu daima.”

Mwishoni  mwa juma lililopita, Pauline Gekul alitimiza idadi ya wabunge 8 kutoka vyama vya upinzani waliotangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai mbalimbali ikiwemo kumuunga mkono Rais Magufuli.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad