Meya wa Manispaa ya Iringa mjini Alex Kimbe kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amedai alishawishiwa kwa shilingi milioni 200 ili ahamie Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuahidiwa kurejea kwenye nafasi yake ya uongozi katika Manispaa hiyo.
Akizungumza na www.eatv.tv Alex Kimbe amesema kuwa, bado anakiamini chama chake cha sasa licha ya baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (bila kutaja majina ya viongozi hao) ambao wamekuwa wakimshawishi kwa muda mrefu na yeye akisisitizia kuwa hawezi kujiunga chama hicho.
Kimbe amesema “Kimsingi (CHADEMA) bado tuko imara Iringa mjini, ni kweli CCM wamekuwa wakinishawishi kwa muda mrefu, lakini nimekataa kwa sababu cheo changu mimi ni kikubwa kuliko Ubunge, kimsingi siwezi kuhama chama changu, viongozi wa CCM walikuja na dau la milioni 200 na kuniahidi kurudi kwenye nafasi yangu nikakataa.”
Mapema mwaka huu aliyekuwa Naibu wa Meya wa Manispaa hiyo Joseph Ryata alitangaza kukihama chama chake cha CHADEMA na kujiunga na CCM na kufanikia kutetea nafasi yake, akishinda kwa kura 15 dhidi ya 13.
Meya Chadema: Nilishawishiwa Kupewa Milioni 200 ili nihamie CCM
2
October 04, 2018
Tags
Alex Kimberly,
ReplyDeleteHiyo ni kashfa kwa Chama Cha Mapinduzi. Kwa tuhuma hizo hukuzipeleka mahakamani?!!!
WanaCCM tusikubali matusi hayo maana wamezoea! Ashtakiwe mara moja!!
#UsirudieKosaKupigiaKuraUpinzaniOvy!
SAHIHISHO LA JINA HAPO JUU:
ReplyDeleteLisomeke hivi:
ALEX KIMBE.