Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe amelalamikia kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa wa Iringa Alli Hapi kuagiza kukamatwa kwa moja ya madiwani wa Manispaa hiyo Selestin Kokumbya kwa kile alichokidai diwani huyo alitekeleza maamuzi ya kikao cha baraza la madiwani.
Meya huyo wa Manispaa ya Iringa amesema tayari wameshamtoa kwa dhamana diwani huyo.
“Mkuu wa Mkoa hakupaswa kumuweka ndani diwani, kwa sababu alitekeleza maagizo ya kikao cha halmashauri na agizo hilo liltolewa mwaka jana na Waziri wa Maliasili na Utalii na tukaamua kumpa kibali kingine cha ujenzi mtu huyo aliyebomoloewa.” amesema Meya wa Iringa mjini.
Aidha Meya huyo alidai Mkuu wa Mkoa wa Hapi kutumia baadhi ya fedha ambazo zilikuwa zimelekezwa kwenye miradi mingine kutumika kwenye ziara yake aliyoipa jina la Iringa mpya iliyodumu kwa siku 20 madai ambayo Mkuu wa mkoa Hapi alitaka aulizwe Mkurugenzi wa Halmashauri.
“Unasema,! mimi nafanya kazi Manispaa,? muulizeni yeye unaniuliza mimi mambo ya manispaa mimi sio Mkurugenzi wa Manispaa mimi Mkuu wa Mkoa nina halmashauri tano na majimbo saba” Amesema Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi kisha akakata simu
Mwishoni mwa juma lililopita wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi aliagizwa kukamatwa kwa diwani wa viti maalum Selestin Kokumbya alikamatwa ijumaa ya wiki iliyopita.