Mgombea wa Uenyekiti Simba ajiondoa

Mgombea wa Uenyekiti Simba ajiondoaAliyekuwa mgombe wa nafasi ya Uenyekiti katika klabu ya Simba ambaye pia ni nyota wa zamani wa timu hiyo, Mtemi Ramadhani, amejiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Mtemi ametangaza kujiondoa leo ikiwa ni siku 9 pekee zimebaki kabla ya tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Novemba 3, 2018.

Mtemi ameweka wazi sababu zilizomfanya aondoe jina lake katika uchaguzi huo kwa kile alichodai kuwa na majukumu mengi na huenda asiwepo tena jijini Dar es salaam hivyo anaogopa anaweza asiitumikie vizuri klabu yake.

"Sababu kubwa kwasasa nina majukumu mengi ninaweza kuhamia Dodoma kwa hiyo nadhani sitaweza kuitumikia vyema klabu yangu ya Simba lakini pia ningependa kuona klabu ina umoja katika kipindi hiki ambacho tunataraji kutetea ubingwa wetu ambao tuliupata msimu uliopita." ameeleza.

Mtemi amefafanua kuwa mara nyingi nafasi hizi zimekuwa zikiwagawa wanachama na kupelekea kuleta makundi ambayo yanakuwa hasimu na kuondoa umoja ambao ungepelekea timu kufanikiwa badala inafanya vibaya.

Pamoja na kujitoa lakini Mtemi ametoa rai  kwa wanachama wa klabu hiyo akiwataka wachague viongozi waadilifu na imara ambao watasaidia kuitoa klabu hiyo katika sehemu moja kwenda nyingine hususani kipindi hiki wanachofanya mabadiliko.

Baada ya Mtemi Ramadhani kujiondoa, mchakato huo unabakia na mgombea mmoja pekee katika nafasi ya Uenyekiti ambaye ni Sued Nkwabi.

Wagombea katika nafasi mbalimbali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad